Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye, ukweli usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu, moyoni mwangu nimeridhia… Nakupenda daima mpenzi!****Ahsante Mungu shukrani kwako mama, pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la mapenzi, ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili chumbani. Penzi lako halichakai daima huzaliwa jipya.******Mapenzi ni upepo, mimi sivumi na kupotea, mapenzi ni mahaba sili nikamaliza, nikimaliza nitakula nini kesho? Nakuahidi kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.