JITAHIDI UISHI KATIKA UHARISIA KATIKA MAHUSIANO

Najua kila mmoja ana malengo na mahusiano yake,,,ni vizuri lakini kuna jambo moja ambalo naomba Mungu akusaidie,,kuna watu wana maneno mengi sana,wanapenda kujionyesha kwa watu,kujitangaza na kujisifia lakini hawaishi sawa na wanavyoongea,,na ndo hapo dada usipokuwa makini unaingia kirahisi na ahadi kibao na sifa

kibao,,kakusifia kumbe mtu huyo ni wa mdomoni na siyo vitendo,,jifunze na anza kubadilika,,tamani kuishi sawa na tamanio la moyo wako,,fanya kweli kama unavyojionyesha nje,,onyesha upendo kama unavyoongea kwa watu,,

kuwa mtu rahisi fanya utu wako wa ndani,,uendane na vile maisha yako unavyotaka yawe,,hii itakusaidia na kukufanya uwe harisi na mpenzi wako atakufura

Hii Hapa Siri Kwa Wanawake Wasaka Ndoa..Chunga Sana la Sivyo Utaishia Kumegwa na Kuachwa

Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema……….Hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu

Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari

Haya hapa  Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake:

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema “Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu”.

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia “Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia”. Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Shukrani za dhati zimfikie mtungaji wa article hii ndg Masanja Mkandamizaji nawasilisha tujadili

AINA YA WANAWAKE AMBAO WATAFANYA MAISHA YAKO KUWA MAGUMU

Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi.

Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.

Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa

Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asiye na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi

Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.

Fahamu Aina ya Kulala Inavyoelezea Kipimo cha Mapenzi Katika Mausiano

Wakati wa kulala si lazima wapenzi wafuate utaratibu ule ule kila mara.Hii inawezekana msimamo wa akili ulivyo kwa wakati huo.Fuatilia mitindo ya ulalaji na maana yake
::
KUKUMBATIANA
Mtindo huu hutumika sana kwa miaka 5 ya mwanzo wa ndoa.Mume huweka miguu juu ya mkewe na mikono kumkumbatia eneo la kifuani.Aina hii hupendwa sana na wanawake kwani hujiona yuko salama
Ni alama ya mahusiano bora ya kimapenzi.
::
KUTAZAMANA
Hukumbatiana lakini baada ya saa 2 au 3 hujibagua na kila mmoja kulala upande wake.Ni alama ya kusaidia kuondoa mkinzano unaoweza kujitokeza.
::
MALIWAZO YA MUME
Hushikana mikono na mke kuweka kichwa chake kwenye mabega au juu ya kifua cha mumewe.
Ni alama ya tafsiri ya mapenzi ya dhati ya mume kwa mke.
::
BARAFU WA MOYO
Mke hupanda juu ya mume na wanaweza kujadiliana mambo mbalimbali.Ni alama nzuri nyakati za maelewano.
::
KILA MMOJA UPANDE WAKE
Ikiwa mmoja kaweka mguu mmoja au mkono kwa mwenzake,mtindo huu hujulikana kama daraja la mahusiano.Si alama ya kutiliwa mashaka
::
USINGIZI BARIDI
Pale wanandoa wanapolala kama wasiotambuana bila kugusana pasipo kujielewa ni alama kuwa wako mbali kifikra.Hutokea pale mvuto usipokuwepo
Hali hii isiruhusiwe ikue.
::
VISIWA TOFAUTI
Wanalala bila ushirikiano kwa visingizio vya kuchoka,ni kama visiwa viwili tofauti.
Chanzo chaweza kuwa matatizo ya kimwili,kiakili au kiuchumi.Hali hii ikitokea mara kwa mara huweza hata kuachanisha wapenzi
::
MGONGO KWA MGONGO
Mtindo huu hujitokeza sana kwa wapenzi.Ingawa wanaweza kupeana migongo lakini wanaweza kuwasiliana.Ni alama ya kawaida na wanasaikolojia wanauita mtindo huu “muda wa kupumzika”
::
MZIGO USIOHITAJIKA
Kila mmoja hulala kivyake na mara nyingi ni kama vile wanandoa wanataka kuonyeshana umwamba.Kila mmoja hamjali mwenzake,,hali hii si ya kawaida ni mbaya sana kwani hutengana kuanzia wanapopanda kitandani hadi kunapokucha.Si ajabu hata kununua vitanda viwili au kulala vyumba tofauti.Wanasaikolojia wanaita hali hii kiburi na jeuri.

Siri za kudumu katika mahusiano ya kimapenzi .

Watu wengi wanatamani kudumu kwenye uhusiano lakini bahati mbaya huwa inashindikana. Mtu ambaye hadumu kwenye uhusiano, si kwamba anakuwa hapendi bali inatokea tu kutokana na sababu mbalimbali. Inatokea kwa sababu, huenda pengine ni kutokana na tabia zake au za mwenzake. Mfano, yawezekana akawa na ‘mdomo’ sana, yawezekana akawa mbinafsi. Au ana hulka ya ugomvi lakini mwenzake hana. Yawezekana akawa na tabia za kuchepuka.

Yawezekana tatizo likawa la mwenzake, Akawa ana tabia zisizompendeza mpenzi wake. Yawezekana akawa mbinafsi, yawezekana akawa na hasira kali au akawa na tabia mbaya ambazo mwenzake ameshindwa kuzivumilia. Kikubwa tu, watu hushindwa kudumu penzini kwa kupishana mambo mbalimbali. Kuanzia tabia, mtindo wa maisha na wengine kutoelewana dhumuni la safari yao.

Mara kadhaa nimekuwa nikisisitiza, unapoanzisha uhusiano na mwenzako lazima kwanza mjue lengo au madhumuni ya huo uhusiano wenu. Mwanamke ajue kwamba uhusiano wao ni wa muda mrefu au wa muda mfupi.

Una malengo au hauna? Vivyo hivyo mwanaume, kwa kinywa chake, kutoka moyoni athibitishe lengo na madhumuni ya uhusiano wake ili mwenzake ajue kabisa kwamba yupo kwenye uhusiano wa aina gani. Baada ya hapo ndio muanze safari.

Na hii ndio siri ya maisha. Ndiyo siri ya uhusiano wote. Mkishajua madhumuni ya safari yenu, kinachofauta ni kukipa umuhimu kipaumbele chenu. Pamoja na kujua kwamba mtakumbana na changamoto mbalimbali katika safari yenu lakini mnapokumbuka umuhimu wa safari yenu, mnatiana moyo. Mnapokutana na magumu yasiyokuwa na mfano, hamkati tamaa. Mnainuka na kusimama tena. Kila mmoja anapomuona mwenzake kakosea, anambebea makosa yake na kumsamehe kulingana na uzito wa safari yao.

Ni kama kiapo. Mnaapa kutoachana, mnaapa kuianza safari pamoja na kuimaliza pamoja. Kifo pekee ndicho kitakacho watenganisha kama kweli wote wawili mtakuwa na nia moja, dhumuni moja la kujenga uhusiano wenu hudumu. Wapenda-nao mnapaswa kuzungumza lugha moja. Kwa pamoja mnapaswa kuazimia namna ambavyo safari yenu mnataka iwe. Mathalan, mnataka muishi maisha ya aina gani? Mnataka kufikia hatua au kufunga ndoa ya aina gani?

Ili muweze kufanikisha safari yenu ya ndoa, mnapaswa muishije? Narudia tena, kusikilizana ndio jambo kubwa sana katika safari yenu. Asiwepo mtu wa kumdharau mwenzake. Mwanamke, amthamini mwenzi wake kuliko mtu mwingine yeyote. Mwanaume, amthamini mwanamke wake katika kiwango cha hali ya juu. Asikubali kuyumbishwa na tamaa za kimwili, asirudishwe nyuma na maneno ya watu na kisiwepo kizingiti chochote cha kumkatisha tamaa.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, suala lenu la ‘utaifa wa uhusiano’ ndio mlitangulize mbele. Muishi mkijua kwamba, uhai wa penzi lenu mmeushikilia nyinyi wawili. Mna kila sababu ya kulilinda penzi lenu kwa gharama yoyote kwani mafanikio ya uhusiano wenu, ni mafanikio ya wote wawili.

Mpendane. Mheshimiane katika kiwango cha juu. Kila mmoja atambue majukumu yake. Mwanamke amtii mwanaume, amheshimu. Mwanaume ampende sana mwanamke. Asimdharau, atambue thamani yake katika nyumba licha ya kwamba mwanaume ndio kichwa cha familia.

Mwanaume asivimbe kichwa. Amshirikishe mwenzake katika masuala yanayohusu maisha na uhusiano wao. Hata ikitokea mmepishana kauli, shukeni. Kila mmoja aongozwe na busara kwamba, ipo njia mbadala ya kuwavusha kwenye mabishano hayo bila kusababisha mtafaruku.

Mwanamke usiwe mzungumzaji sana kwa mwanaume. Mpe faraja pale inapobidi. Farijianeni katika vipindi mbalimbali mnavyopitia. Muanguke na kuinuka pamoja. Asiwepo mmoja kati yenu achukulie changamoto ya mwenzake kama si yake.

Kila mmoja aguswe na matatizo ya mwenzake. Mnapokuwa kwenye furaha, kwa pamoja pia mfurahi. Msiwe na tamaa. Tengenezeni maisha yenu mnayoyataka. Kwa pamoja mtakuja kufurahia ushindi wa safari yenu.

AINA YA WANAWAKE AMBAO WATAFANYA MAISHA YAKO KUWA MAGUMU

Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi.

Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.

Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa

Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asiye na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi

Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.

Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali

Uwe na muonekano mzuri
Wanawake wanapenda wanaume wasafi na watanashati kwa hiyo ukiwa msafi na mtanashati utakua na mvuto kwake. Hivyo utakapoamua kumshawishi kufanya mapenzi itakua rahisi yeye kuwa rahisi kukubali.

Mfanye ajisikie huru

Ni rahisi mwanamke kufanya mapenzi na mtu anayejisikia huru mbaele zake na ambaye yupo huru kuongea na kufanya nae mambo mengine ya kawaida katika maisha. Kwa hiyo ili uweze kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi na wewe njia nzuri ni kumfanya ajisikie yupo huru mbele yako na kasha atakua huru kufanya mapenzi na wewe.
Mfurahishe

Mfanye ajisikie mwenye furaha kila anapokuwa na wewe na atamani kuwa na wewe. Akishajiskia mwenye furaha kila anapokuwa na wewe ni rahisi kushawishika kuwa na wewe kimapenzi.
Mfanye ajione kuwa yeye ni mzuri
Mwanamke anapenda sana na anavutiwa na mwanamme anayeona ubora wake au anayemsifia kuwa ni mzuri.
Mfanye akuamini
Mfanye aamini kwamba hata baada ya kufanya mapenzi bado mtakua pamoja na sio mwisho wa mahusiano yenu au urafiki wenu.
Usiwe na haraka, Mpe muda
Usiwe na haraka ya kumwambia kuwa unataka kufanya mapenzi na yeye bali subiri mpaka utakapoona yupo tayari au anaelekea kukuhitaji.
Mfanye akuone mwaminifu
Mfanye akuone mwaminifu kwa kutomchanganya na wanawake wengine. Usimuonyeshe kuwa una mahusiano na wanawake wengine. Mfanye aamini kuwa unamuhitaji yeye tu.
Mjali kama mwanamke
Mfanye ajiskie kuwa mwanamke. Jaribu kuonyesha kuwa mwelewa, onyesha kuwa unajali, mkarimu na muonyeshe kuwa wewe ni msaada kwake. Mfungulie mlango, mbebee begi au pochi yake n.k.
Onyesha kuwa unapenda kila kitu kutoka kwake
Muonyeshe kuwa unampenda yeye na vyote vyake. Onyesha kuwa umevutiwa na yeye na mambo yake yote na sio mwili wake tuu.

Sababu nne za ugomvi katika mahusiano ya kimapenzi

Kuna baadhi ya makabila hapa Tanzani wanaamini ugomvi katika mahusiano ni sehemu ya upendo, sijui kama ni kweli juu ya imani hii. Japo zipo sababu mbalimbali zinafanya mahusino mengi kutumbukia kwenye ugomvi katika mahusiano ya kimapenzi na sababu hizo ni pamoja;

Masuala ya Fedha
Japokuwa fedha si msingi wa mapenzi, lakini ni kitu ambacho kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo wapenzi katika mahusiano au ndoa hugombana sana juu yake.

Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine siyo, huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya wapenzi hasa wanawake hawataki kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wanaume.

Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya wanaume,na wakati mwingine toka kwa wanawake. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na sharehe nyingine kwa wanaume na baadhi ya wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.

Ni muhimu kwa wenza wawili kupanga jinsi ambavyo fedha zao zitapatikana na kutumika. Vipaumbele vya kufanyika kwanza na kiasi cha kutumika kwajili ya starehe na urembo kwa wanawake kwa mfano.

Suala la Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao wana uhitaji tofauti.

Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.

Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.

Vipaumbele katika Maisha
Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.

Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.

Uaminifu
Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.

Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu lakini huchukua muda mrefu sana.

Mama kuwa makini House Girl Yaweza Kuwa Mke Mwenzio

Hivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba?

Ndugu msomaji wa Muungwana Blog, karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl.

Katika mada hii nimekuwa nikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.

Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa.

WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA: 
Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk.

WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA: 
Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi, kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.

Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.

House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo la nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.

House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa mama mwenye nyumba, nk.

Sasa ukiona house girl anafanya kazi zote nilizosema kuwa hatakiwi kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio umezifanya wewe mwenyewe.

Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe mwenyewe.

Mfanye Aliyekuacha Akutamani tena kwa njia hizi.

Kumfanya mpenzi wako wa zamani kurudiana na wewe si jambo la rahisi kutimiza, haswa kama iwapo ameshachukua hatua ya kusahau yaliyopita na kupata mchumba mpya ambaye wanadate.

jinsi ya kumvutia mpenzi wako wa zamani arudiane nawe
Wakati mwingine, inafaa ujipende wewe mwenyewe zaidi ili kufanya mtu mwingine naye akupende. Inafaa uwashe kitu fulani ndani yako; ili kufungua nishati ambayo inapatikana ndani ya mwili wako ili uweze kuwa mtu tofauti.
Wakati mwingine kama tumevunjwa moyo na kukata tamaa tunasahau kujipenda sisi wenyewe. Dunia yako haifai kuzunguka kwa mtu mmoja pekee. Kumbuka marafiki zako wapya na wa zamani sababu hao wanaweza kukusaidia.

Kuwa jasiri kufanya mambo ambayo hujawahi kufanya mbeleni. Kufanya hivyo kutakupa wewe nafasi ya rahisi kumpata na kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Jaribu kuvumbua upande mwingine wa nafsi yako, na ukigundua kuwa unaweza kufanya mambo kama hayo, unaweza kujiamini kufuata maagizo haya ya kutumia saikolojia ili uweze kumfanya mpenzi wako atake kurudiana na wewe.
1. Tumia saikolojia mjeuko

Mfano
Mpenzi wako wa zamani Ex ameamua kuachana na mambo yenu ya zamani. Hajibu texts zako wala hataki kupokea simu zako.

Kitu cha kufanya
Bila shaka itakuwa wamezoea ya kuwa kila wakati unamfukuzia ama kutaka kujihusisha na kumbabaikia. Lile ambalo utahitaji kufanya ni usijisumbue kuwatext wala kuwapigia simu.

Kama itatokea mkipishana hata usijisumbue kumuangalia machoni. Akikusalimia mambo wewe mjibu tu poa. Hivi hivi unafaa kuwafanyia marafiki zake. Hakikisha ya kuwa unawafanya kana kwamba huwatambui kabisa katika maisha yako. Wewe jifanye mtu wa kawaida kabisa.

Ukifanya hivyo wataanza kushangaa kwa nini umeanza kuwapuuza kwa ughafla. Wataanza kujiuliza kwa nini umeacha kuwatumia jumbe fupi ama kukuona kwa nini siku hizi umeacha kuwa mtu wa kujamiiana. Mwishowe itafikia wataanza kuuliza marafiki wengine kutaka kujua kama umepata mchumba mwingine ama umeanza kudate mtu mwingine.

Owk. Kama unafanya haya yote kumbuka usivuke mipaka. Wakikusalimia jibu salamu zao lakini usiwe wewe wa kwanza kutoa salamu. Muda si mrefu watagundua ya kuwa mchezo umewajeukia wao bila hata wao kutambua.

2. Jipe shughli kwa kuwa buzy
Hakikisha kuwa unajipa shughli zako kila muda. Mwanzo kama mnafanya kazi katika jengo moja ama mnasoma darasa moja hakikisha ya kuwa unafanya shughli zako kama kawaida ili uonekane huna muda na mambo ambayo anafanya…yaani humtambui kama yuko hapo.

Kwa bahati mbaya iwapo itatokea umekuwa na yeye katika sehemu moja jifanye unatext mtu ili mradi usiongee na yeye. Hii itamfanya yeye kujiona mjinga akiwa kando yako sababu wewe upo buzy na shughli nyingine. Kama ni hali mko shuleni, unaweza kumpuuza kwa kujikeep buzy ukiongea na rafiki yako mwingine
3. Usijifanye uonekane mwenye wivu
Mfano
Umemuona mpenzi wako wa zamani akiandamana na mwanamume/mwanamke anayevutia kama vile Justin Bieber/Beyonce wakitembea wakija upande wako.

Kitu cha kufanya
Usionekane mwenye wivu. Jiweke asili yako vile ulivyo.

Unaweza fikiria unapishana tu na wapenzi wawili ambayo huwajui kamwe. Usijaribu kuwakimbia.

Ukijaribu kuwahepa utakuwa unatuma ujumbe kwa mpenzi wako wa zamani ukiashiria ya kuwa bado unawapenda na kumwona yeye na mwanamume/mwanamke mwengine kumekufanya uvunjike moyo. Huku kutawafanya wao kujiskia wako juu na kujiskia raha. Badala ya wewe kuwafanya wajiskie hivi, hakikisha ya kuwa unawapuuza kabisa. Jambo hili litawafanya kuwa na maswali mengi iwapo kama tatizo liko wapi. Kile unachofaa kufanya nikuwapuuza.

4. Badilisha muonekano wako. Kuwa mtu tofauti
Owk najua ushawahi kuskia zaidi ya mara elfu moja kuwa unafaa kubadilisha muonekano wako ili kujionyesha. Well, kufanya hivi kuna umuhimu gani?

Kujibadilisha kunakupa mwonekano mpya na kunakufanya ujiskia vizuri kuhusu wewe mwenyewe. Kufanya hivi kunakupa confidence na kuweza kujiamini kila mahali utakapokwenda.
Kama unaonekana vizuri, kwa kawaida inakuwa kama ni kioo kinachokumulika ndani yako. Hii itatuma meseji kwa mpenzi wako wa zamani kuashiria kuwa maisha yako hayazunguki kwa mtu mmoja pekee ambaye ni yeye.
Iwapo umejibadilisha kabisa, watagundua ya kuwa kuna nafasi ya haraka kwako kuweza kupata mchumba mwingine. Hii inaweza kumfanya Ex wako kuingiwa na hisia za woga wa kukupoteza asilani. Hivyo kuna uwezekano wa yeye kujipendekeza kwako ili mrudiane.
5. Kuwa mtu usiyejali na ujiburudishe
Tumia muda wako ulionao kujiinjoy na marafiki zako. Jumuika na marafiki zako sehemu tofauti, cheka zaidi, enjoy maisha hadi kilele chako. Iwapo ulikuwa na stress ama mkazo wa maisha wakati ulipokuwa ndani ya mahusiano naye na sahizi umekuwa tofauti itaashiria kuwa umekuwa na utofauti mkubwa na kuwa ndani ya mahusiano naye ilikuwa ni balaa tupu.

6. Jifunze kukataa
Ukionyesha kuwa bado unampenda mpenzi wako wa zamani, basi wanaweza kuutumia huu mwanya kukutumia vibaya kwa kuwa hauna uwezo wa kukataa chochote ambacho wanaweza kusema.

Acha kuwa mtu wa aina hii kwa kujikeep buzy na mambo tofauti ya muhimu. Jiheshimu wewe mwenyewe kwa kukataa kutumiwa ovyo. Usikubali kamwe kufanywa mtumwa na mpenzi wako wa zamani. Mwonyeshe kuwa umekuwa tofauti kabisa na mtu ambaye ulikuwa zamani.

Jipe shughli na vitu vyako ili usiweze kutumiwa na ex wako. Hata kama ni kumsaidia na kitu ambacho kinaweza kuchukua dakika 15 unahaki ya kumwambia usoni mwake kuwa haujiskii na kile anachotaka umfanyie.

7. Ingia gym, boresha umbo lako
Kuingia gym ni mbinu moja wapo ambayo unaweza kuitumia kusahau mambo yako ya zamani. Pia kuingia gym kunakupa nafasi kwako kujishepu mwili wako ili uwe na toni ya kuvutia. Pia gym inakusaidia kukupa confidence na kujiamini. Pia gym inakufanya uwe na nguvu zaidi.

Mpenzi wako wa zamani aka ex wako akiona mabadiliko yako ya kimwili, kujiamini na nguvu bila shaka atavutiwa nawe. Labda wakati mwingine anaweza kukuomba kama unaenda gym muende pamoja.

8. Usiwahi kumsifia
Mfano
Wewe na ex wako mmekutana katika birthday party ya rafiki yenu halafu akakusifu kwa mtindo wako uliovalia kwa kusema “Umependeza”. Wewe ni lazima umjibu pia.

Vile unavyotakiwa kusema
Mjibu kwa kumsifia lakini usiingie sana. Unaweza kumwambia “Pia wewe umependeza lakini mtindo wa nywele zako umekaa vibaya na nguo” ama “Hio nguo uliyovaa inaweza kufanya kila mwanamke akuangalie lakini marashi uliopaka yananuka vibaya”

Ok hii itawachanganya kabisa kwa sababu hawakutarajia kamwe kuskia neno ‘lakini’ katika kuwasifia.

Unaweza kuonekana mchoyo lakini hio ni muhimu katika kutimiza lengo lako la kutumia mbinu ya kisaikolojia ili kurudisha akili yake kwako.

Mwisho nikuwa ukitumia mbinu hizi zote kuna uwezekano mkuu wa ex wako kukutizama na sura mpya. Kurudiana na ex wako kutategemea na chanzo chenu cha kwa nini mliachana mara ya kwanza. Labda ilikuwa ni sababu ya kuboeka na mahusiano yenu ama sababu tofauti kabisa.

Design a site like this with WordPress.com
Get started