Upendo wa Mapenzi unahitaji vitu hivi

Asante sana kwa kuendelea kutembelea Muungwana blog siku ya  leo tunataka kuzungumza na wewe mambo muhimu yatakoyokufanya uweze kudumu katika mahusiano.,Ili uweze kudumu katika masuala ya mahusiano ya kimapenzi ni lazima ujue ya kwamba ipo haja ya kujua mambo haya yatakayokusaidia wewe kudumu katika mahusiao hayo.

1. Imani
Upendo unahitaji imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasio onekana unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako imani katika mausiano ni muhimu sana kuaminiana toa wasiwasi kwa mwenzi wako mwamini kuwa amekuchagua wewe hakuna mwingine ukopeke yako.

2. UjasiriUpendo

unahitaji uwe jasiri katika hali zote uajasiri katika kunena ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.


3. Mawasiliano
Upendo unahitaji mawasiliano maana mawasiliano hutengeneza mahusiano bila mawasiliano huku na mahusiano ili ujenge msingi mzuri mzuri wa mahusiano yako unahitaji uwe mtu mzuri katika mawasiliano- mawasiliano yana uwezo mkubwa sana wa kutunza mahusiano hivyo upendo unahitaji mawasiliano.

4. Asante
Upendo unahitaji neno asante kwa mwenzi wako kwa lolote atakalo litenda kwako kama atakupa zawadi asante hasa kwa mpenzi wako ni neno muhimu sana na linaongeza nguvu ya mapendo uwe unatumia neno hili asante kwa mpenzi wako maana upendo unahitaji neno hili ASANTE. Hata baada ya kutoka katika tendo la ndoa sema asante maana ni tendo la ndoa ni matokeo ya mapendo. Hivyo upendo unahitaji ASANTE.

5. Haki
Upendo unahitaji haki unatakiwa umtendee haki mwenzi wako usimyime haki yake ya msingi kumtunza kumpenda na kumtimizia haki zake zote najua unajua haki za mapenzi wako- upendo ili ukomae unahitaji haki iwapo katika mahusiano yenu.

Hizi Hapa Mbinu za Kujitibu Tatizo la Nguvu za Kiume

Tatizo la nguvu za kiume limekuwa ni tatizo kubwa sana, tumekuwa tukishudia michepuko mingi ikiongezeka kila kukicha huku wengine wakithubutu hata kuvunja mahusiano yao hii ni kwa sababu ya tatizo hili, hivyo ili kuweza kuondokana na tatizo hili ipo haja ya kutambua namna ambavyo tunaweza kujitibu tatizo hilo
Zifutazo Njia 13 za kujitibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume:

1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.I kiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.

Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.

Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.

5. Tumia kitunguu swaumu
Chukuwa punje 6  za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.

Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi mbalimbali mwilini.

6. Kula tikiti maji
Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.

Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.

7. Kula ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

8. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

9. Kunywa maji mengi kila siku
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

10. Tafuna mbegu za maboga
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga.

11. Tumia asali yenye mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake. Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari. Au unaweza kuweka vijiko vikubwa vitatu ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote kutwa mara 2 amabapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini.

12. Kunywa chai ya tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.

Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!

13. Tumia unga au juisi ya msamitu
Unga au juisi ya msamitu (mtishamba wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya uume. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari. Msamitu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama pia.

Msamitu pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.

Msamitu unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika nguzu za kiume.

Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, Msamitu unapokuja kukutibu unakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.

Umuhimu wa kusema samahani katika mahusiano ya mapenzi

Wanapokuwa watu wawili kwenye mahusiano, lengo lao linakuwa ni moja ambalo ni kupendana.

Lakini kuna misunderstanding ambayo huwa hahikosi kwa wawili hawa hata kama ni wakamilifu kiasi gani.

Cause no one who is perfect always!! Ila kuna jambo ambalo huwa lipo katikati yao pia ambalo ni kuelewana, na safari inaendelea.

Kwenye mapenzi kuna njia tofauti ambazo zinaweza kuonekana kutatua migogoro inayojitokeza ikiwa ni pamoja na kutumia washauri, lakini kuna dawa moja kubwa sana katika mahusiano na mapenzi kama to say am sorry, samahani ni neno dogo sana lakini matokeo yake ni makubwa sana.

Kusema samahani haimaanishi wewe ni mjinga, au hauna akili au wewe ndio ni mwenye makosa.

Samahani inapunguza mabishano na maneno mengi, inarudisha maelewano ndani ya nyumba.

Inahitaji moyo husiobeba visasi, ina maana kutopiliza kisasi kwa lililotokea hapo awali.

Lakini kwa kuliongelea swala hili ni rahisi sana lakini kwa kulitenda ni vigumu sana, fikiria kama wewe ndio umemkosea mpenzi wako alafu pale pale wewe ndio uombe msamaha,

unafikiri hilo ni rahisi kufanyika? Na vipi kama wewe umekosa na ukaomba msamaha husisamehewe utafanya nini? Will u walk out?? Na ni mara ngapi umetumia neno samahani kwa siku? Na je mahusiano yanaweza kudumu bila samahani??

Bila shaka hakuna mahusiano yanayoweza kudumu bila kujua thamani iliyopoa katika neno samahani, hivyo kusema samahani ni muhimu sana katika mahusiano ili kulifanya penzi lenu liwe bora zaidi.

Njia nyepesi ya kukonga moyo wa mwanamke pasipo gharama

Mawasiliano mazuri kati ya mke na mme ni muhimu sana kwa ajili ya ustawi wa mahusiano ya wawili wapendanao. Inasemwa kuwa kuvunjika kwa mawasiliano pekee katika mahusiano kunasababisha mifarakano au kuvunjika kwa mahusaiano kati ya mke na mme kuliko sababu nyingine.

Wataalamu wa mapenzi na hisia za binadamu wanaeleza kuwa wanawake wanaguswa sana kwa maneno kuliko vitendo. Sauti na maneno mazuri ni vitu ambvyo vinawafanya wawe katika wakati mzuri sana kihisia. Wanaume wao wamefahamika kuwa wanavutwa zaidi kwa kuona kuliko kusikia.

Kwa msingi huu basi ni muhimu sana kwa wanaume walio katika mahusiano ya mapenzi kufahamu siri hii juu ya wenza wao wanawake. Ukitaka kuifanya siku ya mpenzi wako nzuri basi zingatia maneno yako na sauti yako iwe katika kiwango kinachofaa.

Yafuatayo ni maneno manne muhimu kuyasema kila siku kwa mkeo na yataleta mabadiliko makubwa katika mahusiano yenu. Maneno haya yanalainisha moyo,yanajenga uaminifu,yanazidisha upendo,yanaponya majeraha ya mapenzi na yanaleta furaha kati ya wapenzi:

Wewe ni Mwanamke Mzuri
Inawezekana uzuri ni sababu mojawapo ya kumuoa au kuwa naye. Basi hakikisha unamkumbusha kila mara. Wanawake wanahitaji sana kuhakikishiwa kuwa ni wazuri na wanavutia. Ni hatari sana kama hufanyi hivi kwa mkeo,n akuhakikishia wanahitaji kusikia maneno haya. Usipomwambia kuna mtu atamwambia barabarani au kazini na hii ni hatari.

Wanawake wasio ambiwa mara kwa mara kuwa ni wazuri huhangaika sana juu ya kubadilisha mavazi yao na vipodozi. Ikibidi wanaweza wakafikia kuvaa mavazi yasiyo na heshima sana kwa mtazamo wa jamii anayoishi. Hii ni katika kutafuta mrejesho kuwa ni mzuri.

Kama anatumia sana vipodozi na wewe hupendi basi mwambie ni mzuri hasa akiwa asilia,hivyo hahitaji vipodozi vingi.

Umependeza
Hili linaendana na la kwanza hapo juu lakini kupendeza sio lazima uwe mzuri. Uzuri unaweza ukawa wa sura,umbo au tabia zake. Kupendeza ni kutokana na mapambo na mavazi ambayo mtu anavaa.

Kama kuna mambo makubwa ambayo yanawachukulia muda mwingi wanawake wengi basi ni urembo hasa wa mavazi, nywele na vipodozi. Wafanya biashara wajanja wanaweka nguvu zao eneo hili kutoa huduma za wanawake.

Wanawake wanahitaji sana kuonekana wamependeza hasa toka kwa wapenzi wao. Mrejesho huu ni muhimu kwao na kunawafanya wajisikie vizuri , kujiamini na kujiona wa thamani. Mwambie mkeo kila siku asubuhi akitoka nyumbani au kila mnapotoka pamoja. Mwambie kila akibadilisha aina ya ususi wa nywele zake.

Asante
Kwa kweli mke ndiye mtendaji wa mambo mengi nyumbani. Hata kama kuna wasaidizi bado kunahitaji uongozi na bila shaka mke ni kiongozi wa yote haya nyumbani kwa walio wengi.

Utakuta nguo ni safi,chakula ki tayari,watoto wameoshwa na kuvalishwa na mengine mengi. Kuna kila sababu ya kusema “asante”.

Asante ina maajabu makubwa kama ikitolewa kwa jinsi inavyostahili na kwa dhati. Kwanza humfanya anayeambiwa ajione wa thamani sana kwako. Pili humfanya anayefanya aongeze bidii kwa yale anayoyafanya.

Hivyo usiache kushukuru kila siku kwa yale mkeo anayoyafanya. Kunawezekana mengine yakawa si mazuri,lakini hakutakosekana zuri la kushukuru.

Mwambie “Asante Mpenzi” , “Asante Mke Wangu” na maisha yenu yatakuwa mazuri na yenye furaha.

Fanya kwa vitendo pia,mfano nunua hata kitenge tu na umshangaze kwa zawadi. Mwambie “asante kwa kuwa mama mzuri wa watoto wetu” au “Asante kwa kuwa mke mzuri na rafiki mzuri kwangu”.

Nakupenda
Kupendwa ni mojawapo ya vitu ambavyo binadamu anahitaji sana. Chukulia mtoto mfano,toka tukiwa watoto kupendwa ni kitu kinachohitajika sana na kinapokosekana kuna madhara makubwa yanayotokea ikiwemo mtoto kutojipenda mwenyewe na kutojiona wa thamani. Kwa wanawake halikadharika, japo ni wakubwa tayari lakini kasumba ya utotoni imo bado ndani yetu na mahitaji ni yaleyale.

Ukiangalia vizuri mahangaiko yote ya mwanamke juu ya urembo na mavazi utaona kuwa ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Au kujinyima na kuishi katika mwenendo ambao wewe kama mume unafikiri ni vizuri au jamii inafikiri ni vizuri ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Basi kwa kumtamkia kuwa unampenda mara nyingi kadili utakavyoweza inampa kujiamini kwa jinsi alivyo na kwa yale anayoyafanya.

Kumwambia mkeo kuwa unampenda na kuonyesha kwa matendo kunamfanya naye akupende zaidi.

Neno hili likitumika kwa dhati na sio kusema tu lina maajabu makubwa katika kuboresha mahusiano ya wenza wapendanao.

Bila shaka umeelewa vyema, naomba nikutakie utekelezaji mwema katika hilo.

Fahamu jinsi ya kupata mpenzi bora

Unapochagua mpenzi wa maisha unatakiwa kuhakikisha unachagua mpenzi ambaye mtaendana naye kitabia, wengi wa wanawake na wanaume wengi wao utawasikia wakisema mimi nataka mpenzi asiye mlevi wakati huo yeye mwenyewe ni mlevi, kwa kufanya hivi kama utapata mpenzi, ni lazima mapenzi hayo hayatadumu kwa sababu utakuwa umepata mtu ambaye hamuendani kitabia na kihisia pia.

Hivyo ili uweze kupata mpenzi sahihi unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Lazima na wewe uwe bora kwanza.
Huwezi kusema unataka mtu bora wakati wewe mwenyewe siyo bora. Kama unataka mpenzi bora na sahihi kwako unatakiwa kwanza wewe mwenyewe uwe bora kwanza katika kila eneo ambalo wewe linakuhusu ndipo na wewe utakapopata mwenza bora pia. Hii si kwa wanawake tu bali hata kwa wanaume pia kama unataka msichana ambaye ni bora anza kwanza wewe kuwa bora ndipo mambo mengine yatafuta.

Lazima na wewe ujiheshimu.
Utasikia wadada / kwa wakaka wakisema mimi nataka mtu ambaye anajiheshimu, ni heshima gani ambayo unaizungumzia wakati wewe mwenyewe huna heshima hiy?. Kila wakati kumbuka huwezi kupata heshima unayoitaka kama wewe hauna heshima hiyo, kumbuka kila kitu unachokitaka kutoka katika jinsia tofauti ni lazima wewe uwe wa kwanza kuwa na tabia hiyo kabla ya kumuangalia mtu mwingine.

Kama unataka mwenye gari hakikisha na wewe unalo la kwako.
Hii ni kwa wadada utasikiawa kisema oooh mimi nataka mkaka mwenye gari, binafsi huwa najiuliza wewe unalo kama unalo basi una haki ya kusema hivo, kama unataka mtu mwenye gari basi na wewe uwe nalo ili muwe nayo mawili. Acha kujifanya unachagua watu wenye mali wakati wewe hizo mali hauna ni kapuku wa kutupwa. Kumbuka mali hutafutwa.

Ukitaka msomi hakikisha na wewe umesoma
Maara utasikia ooh mimi nataka msomi, mmmh ni usomi upi unaouzungumzia wakati wewe mwenyewe elimu yako huwezi hata kutamka hata mbele ya mtu?. kila wakati acha kujifanya bingwa wa kuchagua vitu ambavyo wewe huna, kama unataka msomi basi hakikisha na wewe ni msomi.

Mwisho naomba kwa kusema maisha ya mahusiano siyo vitu bali ni hisia, ukijifanya bingwa wa kuchagua vitu kuliko kusikiliza hisia zako zinasema nini basi neno ndoa utakuwa ukilisikia kwa waliopo ndoani pekee,

Sababu za wanaume wengi kukimbiwa na wanawake

Imezoeleka katika jamii kwamba wanaume hukimbiwa na wanawake kwa kukosa kipato au alichonacho ni kidogo, au muonekano na maumbile ya mwanaume bila kuzingatia kwamba wanawake huangalia vitu vingine zaidi ili kugundua kama wanaweza kuishi na aina hiyo ya mwanaume.

Zifuatazo ni sababu  zinazowafanya wanawake wakimbie mahusiano na wanaume wenye tabia hizi:-

Kulazimishwa au kusukumwa kwenye maamuzi.
Wanawake hupenda mwanaume mwenye msimamo wake na mwenye kufanya maamuzi na kusaidia wenzie wanapohitahi msaada kutoka kwake pamoja nayeye mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa yeyote. Usisukumwe sukumwe hovyo hata kama ikiwa na mama yako hili huonyesha udhaifu.

Ulevi wa kupindukia.
Sawa, Unywaji wa pombe haujawahi kupingwa ila endapo mwanaume ni mnywaji kupindukia kiasi anaweza akalala hata baa, akaazisha ugomvi au kuzima kabisa haipendezi. Hakuna kitu wanawake wanachukia kama mwanaume asiwejiweza anapokunywa pombe.

Matusi na lugha chafu.
Inawezekana wote kuna wakati huwa tunajikuta tunatumia maneno makali kama matusi na lugha chafu lakini lakini sasa inapofikia 60% ya maneno yanayotoka mdomoni mwako ni machafu, tena bila hata kuzingatia mahali ulipo, haipendezi tena si kwa mwanamke tu. Wanawake huwafurahia wanaume wanaojua nini aseme na akiseme wapi. Lugha chafu na matusi hayatakufikisha popote kwenye sekta hii ya mapenzi.

Kulalamika kuhusu mpenzi wako wa zamani.
Hamna anayejali kwamba mpenzi wako alikua mdanganyifu, alikuchuna au Malaya, kumlalamikia mwanamke wako wa sasa kuhusu mwanamke mwingine kunazidi kukupunguzia nafasi yaw ewe kuwa na mwanamke wa sasa kwa muda mrefu 1) atafikiri licha ya yote, bado unampenda 2) atafikiri hicho ndicho utakifanya kwa anayefuata baada yake kwa maana kwa sasa unalalamika bila upande wa pili kuwepo hivyo waweza kuwa unadanganya na ndicho utafanya na baada ya mahusiano haya.

Mwanaume king’anganizi mwenye kuhitaji zaidi na zaidi. 
Mwanaume analazimisha kupigiwa simu kila baada ya lisaa katika siku? Utadhani isipokua hivyo atafariki, na ukumbuke hapo hata hajawa Boyfriend bado, ndio kwanza anaongea na msichana. Jaribu kutafuta cha kufanya uwe busy kidogo hamna kitu kinakera kama mwanaume ambaye wanawake watafikiri hana kingine cha kufanya zaidi ya kufikiria mwanamke au mapenzi, mpe muda wa kukumiss ili akuze hisia zake kwako inavyotakiwa.

Mtu asiyejali familia wala rafiki zake.
Haitajalisha kabisa hata kama utamfanya yeye ajisikie kama Malkia, kama hujali familia yako hatavutiwa na wewe kwa imani kwamba utamfanyia hivyo nayeye pindi atakapokua mmoja kati ya wanafamilia kama mtafikia hatua ya kuoana. Jitahidi sana uwe na mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka, wanawake huliangalia hilo kwa wakati.

Uongo.
Kusema kweli, uongo kwa wanaume umekithiri, wengi wao huongea na uongo ili wapate wanachotaka vile inaaminika kwao bila longo longo maisha ya siku hizi huwezi kumpata mwanamke, la hasha, endapo mwanamke anagundua umemdanganya kitu, hata kama kilikua kidogo namna gani, imani na wewe inapotea. Hamna uongo mdogo na mkubwa, uongo ni uongo. Na hakuja jinsi ya kujielezea kwanini mtu ulidanganya wakati fulani na sasa unaamua kusema ukweli. Kuwa mkweli wakati wote

Hizi Ndio Amri 10 Za Kumfanya Mwanamke Awe na Furaha.

1. MPIGIE SIMU HATA MARA 1 KWA SIKU KUMJULIA HALI. UKIBANWA SANA, JARIBU KUMTUMIA HATA UJUMBE MFUPI KUONYESHA UNAMJALI.


2. MSIKILIZE KWA MAKINI WAKATI AONGEAPO.

3. CHUNGUZA KWA MAKINI VITU ANAVYOPENDA NA ASIVYOPENDA.

4. MSIFIE/MPONGEZE VIZURI NA KWA DHATI MARA NYINGI IWEZEKANAVYO.

5. MNUNULIE KADI AMA MAUA, WAKATI MWINGINE.SIO LAZIMA VYA BEI MBAYA.


6. MPELEKE KWA CHAKULA CHA JIONI. SIO LAZIMA IWE HOTEL YA NYOTA 5 KILA SIKU. SEHEMU YEYOTE NZURI ITAFAA.

7. KUWA NA UPENDO, SIO FUJO. MAHITAJI YAKE DAIMA YAJE KABLA YA KWAKO.

8. FANYA MAMBO UPENDAYO (KUTAZAMA SOKA, KUOGELEA N.K), PIA FANYA BAADHI YA VITU APENDAVYO KUFANYA YEYE (KUTAZAMA FILAMU, KWENDA KUNUNUA MAHITAJI INAPOTOKEA N.K) ILI FURAHA YENU IKUTANE.

9. MNUNULIE VITU VYENYE MAANA NA ATAKAVYOFURAHIA. SIO LAZIMA IWE IPHONE 6, HATA SHUKA ZURI LITAMFAA PIA.

10. ONANA NAYE MARA KWA MARA KADRI IWEZEKANAVYO.

SIO KILA MPENZI ANAWEZA KUWA MUME AU MKE

MUNGU  ni mwema, ni siku nyingine tunakutana katika uwanja wetu wa mahaba. Hapa tunapata kujifunza, kujadiliana na kuweza kupeana ushauri wa maswala ya mahusiano. Ulimwengu wa sasa una changamoto nyingi.

Ni vigumu sana kumpata mtu sahihi maana kila mtu ana maumivu yake.

Watu wengi wamejeruhiwa, wanajuta kupenda kutokana na waliyoyapitia. Lakini nikutie moyo tu wewe unayesoma sasa, mume au mkeo yupo.

Ni suala la muda tu, lakini ipo siku utakutana naye. Siku hiyo hutaamini kwamba kweli na mimi ninaitwa mke au mume wa fulani maana ulishakata tamaa.

Ulikutana na walaghai wa kila aina, wenye maneno matamu kumbe hawana mapenzi ya dhati.Upande wao wa pili ni hatari.

Mtu unaishi na mwenzako, unamuamini na kumpa moyo wako wote mwisho wa siku anakuja kukutenda. Anakuacha kwenye kipindi ambacho wewe hukujiandaa.

Ulikuwa na mategemeo makubwa na yeye, akili yako iliwaza mbali.

Marafiki zangu mnaosoma hapa, niwaambie tu kwamba msikate tamaa. Kikubwa ambacho kila mmoja wetu anatakiwa kufahamu ni kwamba, maisha ya uhusiano yana siri kubwa ambayo wakati mwingine kuielewa huwa ni vigumu.

Si kila anayekuita baby, sweet, honey na majina mengine kama hayo anaweza kuja kuwa mume au mke wako. Wapo wengi ambao utakutana nao katika maisha ya uhusiano kama sehemu ya kukujenga na kukuimarisha katika safari yako ya ndoa.

Wapo watu watakufuata tu kwa ajili kukufundisha kwamba katika mahusiano kuna matapeli wa mapenzi.

Kuna watu ambao hawana huruma. Kuna watu ambao hawathamini hisia za watu wengine. Kuna watu ambao ni hodari kwa kuumiza mioyo ya wengine.Kweli unaweza kujikuta umezama penzini, ukashindwa kumbaini mapema uliyenaye ni tapeli.

Lakini atakapokuja kujidhihirisha huko mbele ya safari, na ukawa umejitahidi kumfanya awe wako, na ikashindikana basi muache aende.Umeishi naye kwa mwaka mmoja, miaka miwili au hata mitatu, mwenzako akaanza kuleta za kuleta, pambana kumweka kwenye himaya yako.

Pigania penzi lako kama unaweza na itakaposhindikana, kaa pembeni. Ni vigumu kukubaliana na matokeo lakini ifike mahali ukubali yaishe. Kama kupigania penzi lako umepigana sana, umefanya kila linalowezekana kurejesha uhusiano wako lakini imeshindikana, basi huna budi kumshukuru Mungu kwa yaliyotokea.Hakupangwa kuwa mume au mkeo wako.

Alikuwa ni mtu wa kupita. Alikuwa sehemu ya fundisho tu kwako na kujua watu wa aina hiyo walivyo. Anakupa somo hata baadaye utakapokutana na mtu mwingine, uwe makini.

MWANAUME KAMA HUNA PESA NA UNATAKA USIFE MAPEMA USIFANYE HIVI

Kama wewe ni Mwanaume na unamalengo ya kuoa ila huna Pesa, hakikisha usioe mwanamke kisura. 

Kila mwanaume anatamani kumiliki mwanamke kisura kiasi kuwa kila atakapokuwa anapita haoni shobo kumtambulisha mkewe. 

Tatizo linakuje pale huna pesa lakini unataka uweke mrembo ndani. Ndugu yangu, usijidangaje hata siku moja kuwa wapo wanawake wasiopenda pesa na wanapenda maisha ya shida. Hata kama wewe ni Handsome kiasi gani, hakuna mwanamke aliye tiyar kuishi maisha magumu na wewe kisa uhandsome wako. Labda yeye akuowe wewe. Na ukiolewa zipo gharama zake. 

Sasa ukitaka kufa kwa presha na ma stress, kaowe mwanamke mrembo na huku unajijua ni kapuku kama mimi apa

MWANAMKE ZINGATIA HAYA KABLA YA KUOMBA HELA KWA MWANAUME ILI USIJE ONEKANA KICHECHE

Ukweli ni kwamba raha ya mapenzi ni pamoja na kupunguziana makali ya maisha. Na katika kupunguziana uko makali ya maisha ndio matumizi pesa yanapochomoza. 
Kusaidiana ni kwa pande zote iwe kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume au kinyume chake, Ingawa kwa kiasi kikubwa ni wanaume ndio wanawajibika zaidi kutunza wapenzi au wake zao.

Nilichotaka kuwakumbusha wanawake zaidi ni kwamba kweli ni haki yao kutunzwa na waume zao lakini kunavigezo na masharti uzingatie kwa mfano:-

1. Mda gani hasa unapaswa kuomba HELA tangu mahusiano kutokea.
Mapenzi ata wiki bado umeshaomba uchongeshewe kabati LA vyombo.

Haiwezekana kuomba HELA Mara tu mpenzi wako anapokuomba kukutana ata kwa salam tu za kawaida. Mkutano WA kwanza ushaomba HELA ya kusukia mweeh.

2. Usimuombe HELA kwa mume au mpenzi ambayo anatoaga ata bila kuomba, ni uroho.

3. Angalia aina ya kazi anayofanya mpenz au mume na kipato chake ujue aina ya kizinga kinachomfaa, usije kumuova dozi.
4. Weka nafasi ya kutosha kati ya kizinga kimoja na kingine.Isiwe Jana pango ya NYUMBA imeisha, wiki ijayo simu imeingia kwenye ndoo ya maji .

5. Muandalie mazingira mazuri ya furaha kutoka kwako,ikiwezekana baada ya kumpa mavituz yalioenda shule ndio unamkurupusha na kizinga.

6. Kukosa kupo pia sio kila utakapoomba utapata wakati mwingine atakua anasaidia na ndugu pia.
Mume au mpenzi akikuambia cna ujue ana na inatakiwa maisha yaendelelee sio ndio unaanza cm hapokei ppchi hautoi sio poa.

7. Vizingi vikue taratibu usianze tu kuomba laki noo!, anza na kitu cha msimbz then unaangalia upepo ukiona anakuja poa unaendelea usikurupuke tu.

8. Pima aina ya mapenzi unayotoa kwa mtu yana hadhi ya kupewa unachotaka kutokana na ulichotoa. Umenipa mende kafa,laki yangu unaitaka ya nini? Yako wewe ni 5000 kwa services hii.

9. Jitaidi na wewe kumpa chochote ata kama kitatokana na HELA yake nwenyewe poa tu si anajua wewe huna kazi na kipato chako kidogo.

10. Sio lazima kila mkikutana kimwili lazima afungue pochi cku nyingine muagane tu. Kuna watu waajabu mno udhani kila gemu inamtonyo sio ivo.

NB.
Nazungumzia wale wasioelewa ayo apo juu na sijamaanisha wanawake wote.
Ruksaa kuongeza kitu au kupunguza, onesha na namba iliokugusa

Design a site like this with WordPress.com
Get started