Hizi ndio Sehemu 10 Zenye Msisimko Mkali zaidi Kwenye Mwili wa Mwanamke

Kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo.

Mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine.

Kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo.

  1. Kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa.

Jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu.

  1. Sikio; sikio ni sehemu yenye mishipa ya fahamu inayoenda kwenye ubongo, mara nyingi sikio watu hua wanalipuuza sana na kuzani halihusiki lakini naomba nikwambie ni moja ya sehemu inayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe.

Jinsi ya kufanya; anza kwa kumnong’oneza kwa sauti nzito, kisha libusu sikio lake baada ya hapo unaweza kulamba sehemu ya sikio la nje na baadae kuingiza ulimi ndani ya sikio kabisa. hapa msisimko ni mkali sana na anaweza kukukwepa na kutoa sauti kali ya kimahaba.

  1. Ulimi ; ulimi ni sehemu ya mwili ambayo ina mishipa mingi mara mia moja zaidi kuliko ile mishipa ya fahamu ya viganja vyetu. msisimko wa ulimi unasababishwa kumwagika kwa homoni ambazo zinatuletea furaha ya mioyo yetu.

Jinsi ya kufanya; busu tu inatosha kusisimua ulimi wa mtu wako, bahati mbaya kuna watu hawajui kubusu. ukiwa unabusu mtu usipanue mdomo mzima kama samaki mfu… fungua mdomo wako kidogo kisha nyonya lips za juu wakati mtu wako ananyonya za chini na hii ndio busu linavotakiwa kua.

  1. Shingo; hii ni sehemu ya mwili yenye ngozi laini sana ambayo inasisimka hata kwa kuipumulia tu na pua. ni moja ya sehemu nzuri sana kunyonya, kulamba na kubusu.

Jinsi ya kufanya; ukiwa umemkumbatia mtu wako basi busu upande wa kulia au wa kushoto wa shingo huku ukinyonya ngozi la eneo hilo.

  1. Chuchu; wanaume wengi wanatumia sehemu hii kama sehemu kuu kumsisimua mwanamke, ni kweli kabisa tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya ubongo ambayo husisimuka chuchu za mwanamke zikiguswa ni sehemu hiyohiyo ambayo inasisimka kinembe na uke vikiguswa. kwa hiyo ni moja ya sehemu muhimu sana.

Jinsi ya kufanya; tomasa matiti yote ya mwanamke kwa kutumia mikono yako miwili kisha nyonya chuchu yake taratibu huku kama unaing’ata na kuiachia. badilisaha kwa kuchocha chuchu ya kulia na kushoto.

  1. Kiuno au mgongo wa chini; kama umechunguza ni kwamba wanawake wengi husisimka sana wakiguswa viuno vyao ghafla hata wakati wa kukumbatiwa tu. hii ni sababu ya mishipa ya fahamu inayoenda hadi kwenye sehemu zake nyeti hupita huko.

Jinsi ya kufanya; tomasa kama unafanya masaji sehemu ya chini kabisa ya kiuno kabla makalio hayajaanza. hii itamfanya arelax sana lakini pia kuongeza damu kwenda sehemu zake nyeti tayari kwa tendo la ndoa.

  1. Tumbo; tumbo ni sehemu ambayo watu wengi hawaitilii manani sana lakini misuli ya tumbo imeungana na uke moja kwa moja ndio maana baadhi ya wanawake hufika kileleni kwa kufanya mazoezi ya tumbo kitaalamu kama core exercises..

Jinsi ya kufanya; tomasa tumbo lake kwanzia juu kabisa ya tumbo na kwenda tumbo la chini na kisha busu taratibu maeneo mbalimbali ya sehemu ya tumbo na unaweza kumalizia kwa kunyonya kitovu.

  1. Katikati ya mapaja; hii ni sehemu yenye msisimuko mkubwa kwenye mwili wa mwanamke, watu wanaondesha magari wanajua siri hii kwani wakimpakia mwanamke wanatumia njia hii kumsisimua kwa kuweka mkono mmoja kwenye mapaja yake.

Jinsi ya kufanya; shikashika sehemu za katikati ya mapaja kwanzia magotini kwenda mpaka karibu na uke.unaweza fanya hivyo wakati ukiwa unambusu.

  1. Nyayo za miguu; nyayo za miguu zikiguswa hata kwa mtu ambaye sio wa kike zina msisimko sana kama wa kutekenywa hivi na sina msisimko mkubwa kuliko sehemu nyingi nilizotaja.

Jinsi ya kufanya; shika nyayo moja ya mguu kisha kwa kutumia viganja viwili tomasa katikati ya mguu kwanzia kwenye kisigino mpaka kwenye vidole.usitumie nguvu nyingi…

  1. Kinembe [critoris]; hii ni sehemu ya mwanamke ambayo kazi yake ni kuleta msisimko tu na raha kwa mwanamke..eneo hili linazaidi ya mishipa ya fahamu 8000, ni eneo dogo sana lakini shughuli yake sio ndogo. naweza kusema ndio eneo lenye msisimko mkali kuliko yote niliyotaja hapo juu na likiguswa tu mwanamke analoana kabisa.

Jinsi ya kufanya; kidole chako kikubwa cha kinganyani bonyeza na kuachia sehemu hiyo kama mtu anayekagua parachichi pia sugua kwenda chini, juu na pembeni kuangalia muhusika anapenda wapi zaidi pia kama una uhakika na usafi au afya ya muhusika unaweza lamba lwa kuzungusha ulimi sehemu hiyo.

Mwisho; sehemu zote nilizotaja hapo juu ni muhimu sana kwa ajili ya kumuandaa mwanamke japokua kila mwanamke anapata msisimko zaidi kutokana na yeye mwenyewe alivyo yaani mwingine shingo linaweza kua na msisimko wa kawaida likiguswa lakini mwingine ikawa msisimo mkali zaidi.

Dalili 8 Kuonyesha Umependwa Na Mwanaume Lakini Anaogopa Kukuambia

Ukweli usemwe. Kila mwanamume ameumbwa kivyake. Kuna wale ambao mambo yao hupenda kuyaweka wazi na wengine ambao mambo yao hupenda kuyatia kikapuni. Kuna wale ambao hawapendi kujionyesha hadharani na kuna wale ambao mambo yao huyaweka kimbelembele.

Tukija maswala ya kutongoza, kuna mitindo tofauti tofauti ambayo wanaume hutumia ili kufaniikisha lengo lao. Kuna ule msemo unaosema ‘mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani, yaani unaweza kufuata njia tofauti tofauti kufika pahali lakini mwishowe utarudi pale pale sehemu moja, so kwa wanaume kila mmoja ana mbinu yake ya kutongoza. Usiwahi kusema kuwa mwanamume aibu hajui kutongoza akiwa na wewe, labda hio aibu yake ni moja wa mtego aliouweka spesheli wa kukunasa wewe.

So utajuaje kama mwanaume mwenye aibu amekuzimia lakini hataki kuonyesha?

1. Anaingiwa na wasiwasi akiwa na wewe
Ukiona mwanaume anaingiwa na kibaridi ama kupapatika akiwa kando yako ujue ni ishara ya kukuambia kuwa amekuzimia. Hii inatokea wakati mko pamoja halafu anaingiwa na wasiwasi mara anafanya hivi mara vile.

2. Anapenda kuulizia marafiki zako kukuhusu
Mwanaume mwenye aibu akikupenda huwa anataka kukufahamu zaidi kukuhusu. Iwapo atashindwa kuongea na wewe moja kwa moja basi ataanza kuwaulizia marafiki zake kukuhusu. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii ya kuulizia marafiki zako, lile la kufanya nikuonyesha ishara za kuwa uko huru kuongea nayeye wakati wowote ule anapojiskia huru.

3. Anakuwa na tabia isiyoeleweka akikuona
Owk wakati mwingine inatokea ya kuwa mwanaume mwenye aibu anashindwa kustahimili kuonyesha hisia zake hivyo kujaribu kuzificha ili usiweze kuzitambua. Lakini badala ya kuzificha, huibua tabia nyingine ambazo hazina mfanano wa kwake. Usishtuke ukiona akifanyika mambo ambayo si ya kawaida manake wewe ndio chanzo kikuu cha kufanyika hivyo. Yaani utakuwa umempagawisha kiasi cha kuwa anaweza kuanza kuchora miduara kwa mchanga akitumia miguu yake.

5. Anapenda kutabasamu na wewe
Wanaume wote kawaida wakipendezwa na mwanamke huwa wanatabasamu. Lakini kwa mwanaume mwenye aibu aliyekupenda huwa tabasamu lake ni tofauti. Mara nyingi atakuwa akitabasamu lakini mara kwa mara anashindwa kukuangalia usoni. Labda anaweza kukuangalia lakini pindi utakapomuangalia yeye atajifanya anaagalia kando. Hii ni baadhi ya tabia ya wanaume wa aibu hufanya wakati anapojaribu kukupendeza.

6. Anakuwa kimya ukiwa naye
Anaweza kuwa anaongea na marafiki zake sehemu flani, lakini pindi utakapotokea ananyamaza kabisa ama kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka. Hata usishangae iwapo atakataa kujibu salam zako kama umempata katika hali kama hii. Mara nyingi ukimkuta akiwa na maongezi na marafiki zake, atajifanya hata hakuwa akizungumza katika kuchangia maongezi.

7. Anabadilisha mwonekano wake
Ukiona kuwa mwanaume mwenye aibu ameanza kubadilisha mionekano yake kwa kuanza kuvalia nguo tofauti, mitindo mipya ya nywele nk akiwa na wewe, jua hii ni ishara ya haraka kuonyesha kuwa amekuzimia.  Kufanya hivi kwa kawaida ana makusudio ya kukuridhisha wewe. Labda anadhania ya kuwa kuna mtindo fulani ambao akiuvaa unakupendeza.

8. Anagugumiza akiongea na wewe
Mwanaume huyu hujamsikia akikwamakwama wakati anapoongea lakini ghafla unamskia akigugumiza anapoongea na wewe. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anaishiwa na maneno ya kukuambia na inakuwa vigumu kwake kuyatoa ama kutafuta maneno ya kukuambia.

So ni kitu gani kinachowafanya wanaume aina hii kuwa spesho kwa mwanamke?
Kuna wanawake ambao wanapenda wanaume ambao ni wa aibu kwa kuwa hawana mambo mengi. Lakini usishangae kumwona mwanaume aina hii akikuapproach akutoe mkale bata pamoja. Pia aina hii ya wanaume itafikia wakati fulani wanaweza kukushangaza kwa kufunguka na kugundua kuwa ilikuwa tu ni baadhi ya mbinu waliyotumia kukuteka kimapenzi.

Jinsi Ya Kuwaepuka Wanaume Wanaokutongoza Ilhali Unawachukia


Ishawahi kutokea kwa kila mwanamke ya kuwa kuna mwanaume mmoja ambaye anakutongoza ilhali unamchukia. Halafu mbaya zaidi ni kuwa mwanaume kama huyu haskii kabisa, kila ukijaribu kumkataa ndivyo anavyozidi kukuapproach.
Mara nyingi huwa inaanza hivi. Anakuapproach, anakutongoza halafu unamkubali kiasi cha kuwa unataka kumsoma akili yake. Baada ya kutoka out ama deti mara kadha ukakuja kugundua kuwa mwanaume kama huyu ana matatizo flani ambayo wewe binafsi hukuyapenda. Unajaribu kumkaa mbali lakini unamwona hataki. Unajaribu kila mbinu za kumtenga lakini yeye anasistiza.

Well. Wakati ni sasa wa kumwambia akuache kabisa kwa kutumia mbinu zifuatazo.

#1 Mwambie kwa upole kuwa hujiskii na yeye. Kama umegundua kuwa huyu mwanaume anayekuvizia ana matatizo lakini si tishio kwako, basi kumwambia ukweli ndio muhimu. Mwambie kuwa yeye ni mwanaume mzuri *hata kama sivyo*, lakini huko interested na yeye ndani ya moyo wako.

Akiuliza ni kwanini, mwonyeshe utofauti wenu. Unaweza kumwambia kuwa wewe ni mtu unayependa kuparty ilhali yeye ni mtu anayependa utulivu, ama unaweza kumwambia wewe ana uraibu flani ilhali wewe huna. Anaweza kuuliza iwapo munaweza kuwa marafiki, lakini iwapo unataka pia kuhepa unaweza kumwambia kuwa itakuwa vibaya kuwa marafiki kwa kuwa tayari mumeanza vibaya.

#2 Usijibu simu wala texts zake. Wakati mwanaume kama huyu amezuzulika na wewe, ama pia kuna wanawake wengine anaowaaproach, si lazima umpe maelezo kama ya hapo juu, bali unaweza kumwondoa polepole kwa maisha yako.

Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamuingiliani.

#3 Mblock katika mitandao ya kijamii. Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mbaya, na unaona si tishio kwako, basi angalau fanya kumdelete.

Kumuweka katika contacts zako kutampa hisia ya kuwa nyinyi wawili mna connection aina flani, aidha ya kibinafsi au kikazi, hivyo kuona kuwa ni haki yake kuwasiliana na wewe.
#4 Badilisha namba yako ya simu. Najua utahisi vibaya kubadilisha namba yako ya simu, lakini kama mwanaume atakuwa anaendelea kukupigia simu na kukutext mara kadhaa kwa siku, ilhali tayari amejua kuwa huko interested na yeye, basi itakuwa jambo la kufanya ili kujiokoa.

Pindi utakapojeuza namba yako, usijaribu kuiweka sehemu yeyote online, kwa sababu huyu mwanaume ama rafiki yake anaweza kuiona. Pia hakikisha kuwa marafiki zako hawapeani namba yako ya simu kwa yeyote.

#5 Jifanyishe kuwa una boyfriend. Wakati mwingine huyu nuksi akifikiria kuwa una boyfriend, atatulia na kuachana na wewe kabisa na kufuata mwanamke mwingine. Hii ni kweli haswa iwapo huyu nuksi ni mwanaume mwoga ama mwenye haya.

Ukianza kumwambia huyu mwanaume nuksi kuwa wewe hauko single, basi mwisho ataenda zake. Kama hatareact na hizi habari mpya, unaweza kutafuta mwanaume mwenye miraba halafu umfanye kuwa ni boyfriend wako wakati unamwona yuko karibu.

#6 Tafuta mbwa. Hili si jambo la haja kwa kila mmoja, lakini kama una kazi na uko na nyumba yako, na unasumbuliwa na wanaume aina kama hii, basi inakufaa ufuge mbwa. Ukiwa na mbwa mkubwa halafu mwanaume kama huyu afikirie kukutembelea basi atajipanga coz mbwa katika nyumba yako atakuwa akikulinda wakati wote.
#7 Safiri na marafiki zako.  Kama unaona mwanaume huyu nuksi anayatishia maisha yako, basi si vyema kusafiri ukiwa pekeako. Badala ya kusafiri pekeako, tembea mjini ukiwa na rafiki yako ama tembea ukiwa katika kikundi na rafiki zako.
Ili mradi usitembee pekeako wakati wote basi utakuwa umeponea kusumbuliwa na mwanaume aina kama hii.

#8 Tafuta barabara mbadala za kwenda shuleni, kazini nk. Kwa wale ambao wamezoea kutembea, ile barabara ya kawaida unayoitumia kutembea shuleni, kazini, ama katika shughli zako za kawaida zinaweza kukuelekeza moja kwa moja hadi kwa huyu mwanaume nuksi sehemu anakoishi, kazini ama sehemu ambazo anatembelea mara kwa mara. Kama anaweza kuwa na nafasi, anaweza hata kujiweka barabarani maksudi ili tu apatane na wewe.

#9 Vaa kofia na miwani. Kuvaa miwani na kofia wakati mwingine husaidia kujificha kutokana na mwanaume aina kama hii. Mwanaume huyu hawezi kukusumbua iwapo hataweza kukutambua wewe. So ni muhimu kuvalia hivi iwapo unaenda sehemu ambazo unaweza kutana na wanaume kama hawa.
#10 Mjulishe mwajiri wako na wenzako. Kama haijubi simu zake, wala kumtext ama online, kuna uwezekano mkubwa jamaa kama huyu kuweza kwenda katika sehemu  yako ya kazi. Kama unashuku kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwake kuja sehemu unayofanya kazi basi ni bora zaidi kumjuliza mwajiri wako na wenzako ili wakati ambapo atajaribu kuja sehemu unayofanya kazi ataambiwa aende zake.

Bydaway, kama unadhania mwanaume kama huyu anayekusumbua hajui sehemu unayofanya kazi basi unakosea, wanaume kwa kawaida wana taaluma ya juu ikiha kwa kutafuta kile wanachotaka.

#11 Tafuta mwanaume mwengine akusaidie ili amalize mawasiliano yenu. Tofauti na wanawake, wanaume huwa wanareact haraka iwapo utawaomba usaidizi kama unasumbuliwa na mwanaume mwingine. Kama huyu mwanaume anakusumbua bila kukuacha basi unaweza kumwambia mwanaume unayemwamini haswa kama ni ndugu yako, mtu unayehusiana naye ama rafiki yako wa kiume.

Wakati wa kuchagua mwanaume kama huyu hakikisha kuwa ana uwezo mkubwa wa kushawishi ili aweze kumwambia huyu mwanaume msumbufu aachane na wewe kabisa. Hakikisha pia huyu mwanaume ana nguvu na uwezo wa kukabiliana na mwanaume kama huyu.

#12 Wahusishe polisi. Hii ndio suluhisho la mwisho kabisa na linapaswa kutumika katika hali zile nzito kabisa haswa kama umeona kuwa mwanaume kama huyu amekuwa tishio kwako na umejaribu kila hatua umeshindwa. Kama umeamua kuwapigia simu polisi jipange tayari kutoa ushahidi wote ambao utahitajika kama vile jumbe alizokuwa akikutumia.

So haya ndio mambo ambayo yanaweza kutumiwa kuhakikisha kuwa unakabiliana na mwanaume yeyote aina hii.

Hivi Ndivyo Mwanamke Anavyoweza Kufanya Mpenzi Wake Atembee Na Mashosti Zake

Maisha ya kimapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kwani kuna changamoto nyingi zinazoweza kujitokeza kiasi kwamba usipoangalia unaweza kuishia kusema hutakuja kumpenda mtu, heri uishi peke yako!

Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Lakini naomba leo niseme kwamba, wapo watu wanajitakia kusalitiwa na hapa nawazungumzia wanawake.

Kuna wanawake ambao wana wapenzi au wako kwenye ndoa lakini wanafanya mambo ambayo yanawafanya wasalitiwe kirahisi.

Unamkuta mke anachekelea mumewe kuwa na ukaribu na shosti wake, anajipenda kweli huyu? Hili ni tatizo na ndiyo maana leo nimeona nizungumzie mambo manne ambayo ukiyafanya lazima mumeo ‘atoke’ na marafiki zako.

Moja; ukaribu wa mume na marafiki wa mke. Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao. Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?

Sisemi uanze kumfikiria tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo wamemchukua. Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia.

Pili; mawasiliano ya mume na marafiki wa mke. Sisemi marafiki zako wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana kwa mambo gani?

Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea, walahi utaula wa chuya!

Tatu; mke kuanika siri za mumewe. Kuna hii tabia ya baadhi ya wanawake kuwasimulia mashosti zao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba! Eti unamkuta mke anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa faragha.

Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo. Kimsingi hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.Nne; mwanamke kutochukua nafasi yake. Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.

Hili liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza kumfanya akusaliti.

Hata kama wapo wanaopatiwa kila kitu lakini wanachepuka, hao ni wale wasioridhika na ni wachache. Wewe chukua nafasi yako kama mwanamke halafu hakikisha unaziba mianya ya mumeo kushawishika kwa wengine.

Mambo yatakayomfanya mpenzi wako asikuache kamwe.


Upendo ni kitu ambacho hakizuiliki. Napale patakaposhikilia ule upendo ipasavyo ndo husikii wala huoni utakaloambiwa juu ya akupendaye. Matendo mbalimbali yanayofanywa na wale wapenzi moja kwa moja huchochea upendo wa moyoni ambao hudumu milele, ndio hapo utasikia keshapewa madawa, mara mke wake kamkalia kila atakachoomba lazima apewe na mengine  mengi ambayo umekumbana nayo au kuyashuhudia kwa watu wengine.

Moja kwa moja niende kwenye hivo vichochezi kama ifuatavyo:
Kusikiliza na kua mshauri mwema kwa mwenzako. Iwe ni kuhusu familia yake au mipango yake ya baadae au kimasomo, kikazi na hata kibiashara. Ikumbukwe kuwa mafanikio ya mmoja ni chachu ya maendeleo mazuri  hata mtakapokua katika familia.

Kujishusha panapotokea kutokuelewana (yaani kuwa mwepesi wa kuomba msamaha). Majibizano siku zote hayajengi hasa mnapokua mna hasira au mmoja kati yenu ana hasira.

Neno ahsante ni dogo sana ila lina couragement kubwa saana, Ukipongezwa na hata unapopewa pole shukuru. Unapopewa chochote na mwenzako iwe ni ushauri, maoni, mawazo mapya juu ya miradi mbalimbali au kazi huna budi kushukuru.

Mwepesi wa kusamehe na kusahau. Vilevile mwelekeze mwenzako pale alipokosea ili siku nyingine kitendo hicho kisitokee. Usiwe mwombaji mzuri wa msamaha huku wewe hautoi.

Msifie mwenzako anapopiga hatua ya maisha anapokua katika muonekano mzuri n.k Usisubiri jirani amwambie. Tena hapa muwe makini sana maana ni rahisi kwa mwingine kuvutika upande wa pili kwa ajili yakusifiwa(Kusifia kunajenga  picha ya kujali) japokua sio wote wanamaanisha.

Kuwa mkweli na mwaminifu katika mahusiano yenu

Usisubiri matukio maalum ndo utoe zawadi kama vile birthday, valentine day  n.k, Mpe wakati wowote unapokua na uwezo wakumpa.

Usimuulize mpenzio anataka zawadi gani. Siku zote zawadi ni kitu ambacho mpokeaji hakijui na wala hatakiwi kukijua kabla hujampelekea. Kuna zawadi nyiingi sana ambazo unaweza mpa mwenza. Na kupitia muda wa urafiki wenu naamini utaweza kujua walau nusu kama si robo tatu ya vitu anavyovipenda. Ila jitahidi uwe ni muibuaji wa vitu vipya sio vilivyozoeleka.

Natumaini kwa kiasi fulani vitu kama hivyo kutoka kwa mwenza wako  vimekufanya au vinakufanya umpende zaidi. Au ukosaji wa vitu hivi kwa mwenzako vimekufanya mshindwe kuendelea kua katika mahusiano au kuvunjika moyo. Jiheshimu na pia muheshimu mwenzako pamoja  na hisia zake, mjali, mthamini, mtie moyo, mrekebishe anapofanya ndivyo sivyo na lingine ni kuombeana Baraka za mwenyezi Mungu zikae nanyi nakuwaongoza katika kila jambo.

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Atabasamu Na Apende Kuwa Na Wewe Wakati Wote.

Kama tunataka kutongoza mwanamke, kuwafurahisha ama wajiskie huru mbele zetu huwa tunatumia mbinu ya kuwafanya watabasamu. Kutabasamu ni njia moja wapo ya kuondoa misongo ya mawazo, uchovu, na hata kuondoa uzee. Ndio maana wazungu walikuja na ule msemo wa laughter is the best medicine.

Kabla hatujaingia katika swala la jinsi ya kumfanya mwanamke atabasamu, lazima tufahamu ya kuwa kuna tofauti kati ya kutabasamu na kucheka. Kucheka ni pale ambapo utakuja na mizaha ya zee comedy ili mwanamke acheke ilhali kumfanya mwanamke atabasabu utakuja na mbinu ambazo tutakueleza muda mfupi.

Tukija katika swala la kumfanya mwanamke atabasamu lazma ufahamu kuwa hauhitaji kufikiria sana. Lazima uwe natural. Sababu pindi utakapoanza kufikiria mbinu za kutumia kumfanya mwanamke atabasamu basi atakugundua. Hivyo la kufanya ni kuhakikisha unapumua vizuri na unatumia mbinu za kujiamini.

#1 Mpogeze.

Hii ni mbinu inayotumika sana na bado inafanya kazi. Lakini kabla hujatamka neno unapaswa kuanza na tabasamu. Weka tabasamu na umwambie maneno kama, “Wow! Leo unaonekana mrembo sana.” Ama unaweza kumwambia, “Hii nguo uliovaa leo imekupendeza sana”

Maneno kama haya hujayapangia, yanakuja yenyewe kulingana na mandhari ambayo mko. Mbinu hii ambayo imekuwa ikitumika tangu zamani hufanya kazi vizuri.

#2 Mnunulie kitu.

Hapa unafahamu ya kuwa lengo letu ni kumfanya mwanamke atabasamu na wala si kumtongoza. Kama unataka kumtongoza awe mpenzi wako ingia hapa. Ok, tukirudia kwa hoja yetu ni kuwa mwanamke huyu haimaanishi kuwa unapaswa kumnunulia zawadi, la. Hapa namaanisha unamnunulia kitu kama vile mumeenda klabu ukamnunulia kinywaji ama umeenda kwa mkahawa ukamnunulia vibanzi, chokoleti na kadhalika. Hii ni njia murua ya kumfanya atabasamu.

#3 Msaidie.

Huku ni kumsaidia pale ambapo anashindwa kufanya ama anahitaji msaada. Hii ni kuanzia kama anataka usaidizi wa kubebewa mizigo kwa gari, kumtengenezea aeaeri yake ya tv, kumsaidia kupiga picha akiwa na marafiki zake. Kiufupi ni yale mambo madogo madogo tu. Si lazima ufanye jambo la kuchekesha ndipo umwone mwanamke atabasamu.

#4 Shika macho yake.

Kumsuka mwanamke kwa kutumia macho kunatambulika kama mbinu fioa ya kutongoza mwanamke. Mbinu hii pia inakuwa na uwezo mkubwa wa kumfanya mwanamke atabasamu. Ukijifundisha mbinu za kutongoza kwa kutumia mwanamke itakuwa silaha kubwa katika nyaja ya utongozaji.

Mbinu hii unaweza kuitumia katika klabu, hotelini ama kwa chumba tu. Kile unachohitajika nikuangalia macho yake kwa sekunde tatu halafu uangalie kando. Fanya hivi kwa muda wa kama dakika kumi na tano hivi na mwishowe unaona amekuwa interested na wewe na zaidi utamfanya atabasamu.

#5 Tafuta mwanya mowote ili ujitolee kwake.

Unaweza usipate nafasi ya kumsaidia na kitu, lakini kuna watu wengine wengi katika hii dunia. So mahali popote pale ulipo, makinika kutafuta mwanamke ambaye atakuwa anatatizika kufanya jambo. Hii pia itakusaidia pakuu kuondoa uoga wakati ambapo itafika ule wakati wa kuapproach mwanamke kumtongoza.

#6 Mwambie kuwa anafaa.

Well, hapa utamweleza anafaa kwa njia gani. Hii itategemea na vile ambavyo unamchukulia mwanamke huyu. Unaweza kuwa mumetoka matembezi na mumefurahia hadi jioni. Halafu wakati mnaagana unamwambia, “Wewe unafaa” Maneno haya bila shaka yatamfanya atabasamu.

#7 Kuwa gentleman. 

Kuwa gentleman ni kama vile ambavyo tumeeleza katika hoja ya #3. Gentle ni tabia za utu ambazo wanawake wengi hupenda. Ukimfungulia mlango, kumsaidia kuvuta kiti akae ni baadhi ya tabia za gentleman. Wanawake bila shaka watatabasamu ukiwa na tabia kama hizi.

#8 Kuwa romantic.  

Kando na kuwa gentleman, unafaa kuwa romantic muda wote ambao mtakuwa pamoja. Kuonyesha kuwa romantic ni pale ambapo unamwita katika mazingira ambayo kuna mishumaa, maua, chokoleti na kadhalika. Vitu hivi kwa mwanamke hufanya kazi sana.

Pia unaweza kudance na  yeye. Weka nyimbo ya kimahaba katika simu yako na uanze kudance na yeye polepole bila kukurupuka.

#9 Mshike mkono.

Wakati mnakutana na wazazi wake ama wazazi wetu ama kuwa katika hali ya wasiwasi, unaweza kuukaza mkono wake pole pole. Kufanya hivi kunakuwa na maana nzito ajabu. Hii ni ishara ya kumuonyesha kuwa ‘ijapokuwa hatuwezi kuongea sahizi, niko na wewe na wala siwezi kukuacha’

Finally ni kuwa kumfanya mwanamke atabasamu lazima ile hatua ya kwanza ni kumfanya ajihisi vizuri. Baada ya hapo, chochote kinaweza kufanyika. Hii ni mbinu mora zaidi ya kuanza mahusiano mazuri na mwanamke.

Hii Hapa Siri Kwa Wanawake Wasaka Ndoa..Chunga Sana la Sivyo Utaishia Kumegwa na Kuachwa

Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema……….Hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu

Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari

Haya hapa  Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake:

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema “Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu”.

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia “Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia”. Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Shukrani za dhati zimfikie mtungaji wa article hii ndg Masanja Mkandamizaji nawasilisha tujadili

Siri Muhimu Unazotakiwa Kuzijua Kuhusu Wanawake

Wanawake wana siri nyingi sana mioyoni mwao na kwa kawaida huwa hawawezi kuonesha hisia zao za ndani moja kwa moja. Ni watu ambao mara nyingi hupenda kuwasilisha vilivyomo ndani yao kwa ishara.

 Kwa mtindo wa maisha ya wanaume wengi wa sasa ni vigumu kusoma ishara hizo na kujua mahitaji ya mwanamke husika. Bahati mbaya ni kwamba, ukienda kinyume na mahitaji yao, utashangaa kila siku mnaingia kwenye mikwaruzano isiyo na msingi.

Wiki iliyopita nilieleza machache, leo tunaingia katika sehemu ya mwisho. Hebu fuatilia kwa makini ujue mwanamke anapenda vitu gani hasa ili uweze kuishi naye kwa amani.

KUSIKILIZWA

Ukitaka kumpatia mwanamke, msikilize. Kumbuka wanawake wengi wana hulka ya kuongea sana! Ndivyo walivyo.

Wakati fulani, mwanamke anapenda kuzungumza mambo fulani na mwanaume wake.

Pengine anapenda kumshauri au kujadiliana naye jambo fulani; huenda ana mawazo mazuri lakini mtindo wao wa kuongea sana unaweza kukatisha tamaa. Usifanye hivyo. Mpe nafasi.

Msikilize kwa makini, mwishowe unaweza kupata manufaa makubwa kutokana na maneno yake. Amini usiamini, hata katika mambo yanayohusu mafanikio, ukimshirikisha mkeo, huwa na mawazo mazuri yanayochochea kuifukuzia ndoto yako.

Ukiachana na hilo, mwanamke anaweza kukuambia, hapendi mavazi yako – hapendi nguo fulani unayovaa, labda kwa hoja kuwa haikupendezi! Usimdharau. Sikiliza hisia zake.

Kumbuka upo kwa ajili yake, anaweza kujiuliza, kama anakuambia mavazi hayo si mazuri kulingana na umbo lako na ung’ang’ania, unamvalia nani huko nje? Msomaji mmoja aliwahi kuniambia: “Yaani kaka Shaluwa, mume wangu ananishangaza sana.

“Anapenda kuvaa suruali za vitambaa, pana na mashati makubwa kama Mzaire. Nimeshamwambia mara nyingi kuwa sipendi na hapendezi, lakini bado analazimisha kuvaa. Ananinyima raha sana, maana hata nikiongozana naye, nakuwa kama nipo na mtu mzima!”

Unaweza kuona namna gani wanawake wanavyokereka na mambo madogo tu lakini wakiyapa uzito
wa hali ya juu.

MSIMAMO

Wanawake wanapenda mwanaume mwenye kujiamini na kusimamia msimamo wake. Unaweza kushangaa lakini wakati mwingine mwanamke anaweza hata kukuweka kwenye mtego; mnakubaliana jambo lakini baadaye anajifanya kukupinga ili kuona msimamo wako.

Wanaamini katika mwanaume anayejielewa na asiyeyumba wala kuyumbishwa. Kwamba, mwanaume wa aina hiyo ni rahisi kufikia ndoto za familia – yeye kama kiongozi wa nyumba.

ZAWADI

Si lazima ununue gari jipya na kumpelekea kama zawadi. Kumchagulia wimbo mzuri redioni, kadi yenye mashairi mazuri ya kimapenzi, bangili, vipodozi na vitu vingine vidogovidogo huwafurahisha sana wanawake.

MTOKO

Hata kama ni mara moja baada ya miezi miwili, ukitoka na mwenzako na kwenda naye kupata chakula cha jioni mgahawani huongeza mapenzi. Kwa mwanamke ni jambo kubwa lenye thamani sana.

NJIA YA KUMTONGOZA MWANAMKE AWE MPENZI WAKO .

Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote. Hapa kuna njia 10 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo nae…

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia “hisia” kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu, kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri, kuwa nini uchokuwa ukizungumza.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza naye kwa majibu yasiyo na anayokuwa akikujibu, na kama kwa bahati mbaya ukonaye karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu… kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu “Ucheshi/vituko si mapenzi”. Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asichikie au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi katika mzungumzo yenu. Bali cha zaidi jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza “wewe umekulia wapi?”, uliza “unaonekana kama hujakulia maeneo haya!” Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako – zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke si vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake… kisha rudi utoe maoni yako.MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli – yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana

Siri ya kudumu katika Mahusiano ya Ndoa .

Sabrina Adriani ambaye ni mtafiti wa masuala ya mahusiano ni miongoni mwa wanawake ambao wamedumu miaka mingi katika ndoa.

Na alipoulizwa ni kwanini ameweza kukaa kwa miaka mingi katika ndoa bila kufarakana na mumewe alisema “siri kubwa ambayo imenifanya nidumu katika ndoa ni kwamba niliweza kutumia muda mwingi zaidi ya miaka kumi kuweza kumfahamu mume wangu vizuri, ninaposema kumfahamu hapa nina maana ya kwamba kujua tabia zake zote kiundani zaidi, nilifanya hivi ili kujua ni kipi hapendi na kipi anakipenda? baada ya kujua hivyo nikaweza kuishi naye vizuri maana wanasema ya kwamba mkimjua mbwa jina hakusumbui.

Lakini sikuishia hapo nikaweza kutenga muda wangu angalau mara tatu kwa wiki kusoma saikolojia ihuduyo mahusiano hicho ndicho kitu kikubwa ambacho kimenisaidia.

Lakini sabrina hakuishia hapo aliendelea kusema ya kwamba moja ya sababu kubwa ya kufa kwa ndoa nyingi barani Afrika na duniani kote ni kutoshukuru kwa chochote ambacho amekipewa na mumewe, akatoa mfano ya kwamba utakuta mtu ameletewa zawadi na muwewe lakini kwa kuwa hajaipenda zawadi hiyo, utashangaa majibu ambayo yanamtoka kinywani mwa mwanamke huyo baadala ya kushukuru, utakuta mtu anasema ni kitu gani hiki ambacho umekileta? Na majibu mengine mengi kama hayo

Kwahiyo hiyo ndo sababu kubwa ya kufa kwa ndoa nyingi, hivyo baada ya mimi kufunga ndoa hata zawaida iwe nzuri au mbaya nilikuwa namshuru muwe wangu kwa kile ambacho ameniletea ili kumridhisha mume wangu, na nilifanya hivyo ili kumthihirishia ya kwamba nimefurahi kwa zawadi aliyoniletea pia najivunia kuwa na yeye, pia nilifanya hivyo kila mara ili kutomkatisha tamaa na azidi kuelewa ya kwamba mimi ni mwanamke tofauti na wanawake wengine.

Lakini kabla hajamaliza kuzungumza siri ambazo zilimfanya kukaa kwenye ndoa muda mrefu, alizungumzia muda mzuri ambao unafaa katika kufanya mazungumzo na mwezi wako, katika hili alisema ” katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa miaka ya nyuma na watu ambao wanahusika na masuala ya saikolojia ya mahusiano waligundua ya kwamba mwanamke nyakati za asubuhi huwa hana uwezo mkubwa kuzungumza maneno mengi, ila nyakati za usiku huwa ana uwezo kuzungumza maneno mengi sana ambayo ndani ya maneno hayo huwa ni jazba au kwa maneno mengine tuite maneno yasiyo na mpangilio.

Na kwa upande wa mwanaume ana uwezo wa kuzungumza maneno mengi sana wakati wa asubuhi kuliko nyakati jioni au usiku, hii ni kutokana na shughuli nyingi ambazo mwanaume huyo huzifanya kwa siku nzima, hivyo mwanaume anahitaji muda mzuri nyakati za jioni kwa ajili ya kupumzika.

Hata kwa kuwa wengi hawajui siri hii utashangaa mwanamke anamfokea mwanaume wake nyakati za usiku na kwa kuwa mwanume kama nilivyosema hapo awali ya kwamba mwanaume nyakati za jioni au usiku huwa hapendi kuongea utashangaa mwanamke huyo anapigwa na mumuwe.

Hivyo basi baada ya kujua siri hii nikajua ya kwamba wakati mzuri ambao utatufaa mimi pamoja na mume wangu kwa ajili ya kuzungumza ni wakati wa asubuhi, muda huu ni mzuri kwa sababu mume wangu akili yake inakuwa imetulia na anakuwa ana uwezo mzuri kuzungumza. Hivyo nyakati hizo za asubuhi huwa natumia kuzungumza naye kuhusu masuala ya mafanikio na familia kwa ujumla.

Baada ya kusema hayo akawasisitiza wanandoa wote waweze kuyazingatia hayo ambayo yamemsaidia yeye kuweza kudumu katika ndoa.

Bila shaka naamini ya kwamba umejifunza mambo mazuri kutoka kwa mwana mama Sabrina, hivyo nikusihi na wewe uweze kuyazingatia hayo katika mahusiano yako ili kuweza kutengeneza mahusiano yaliyo bora kila wakati. Na mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane siku nyingine.

Design a site like this with WordPress.com
Get started