HIZI Ndio Sehemu 10 zenye Msisimko Mkali zaidi Kwenye Mwili wa Mwanamke

Kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo.

Mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo  cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine.

Kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo.

1. Kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa.

Jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu.

2. Sikio; sikio ni sehemu yenye mishipa ya fahamu inayoenda kwenye ubongo, mara nyingi sikio watu hua wanalipuuza sana na kuzani halihusiki lakini naomba nikwambie ni moja ya sehemu inayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe.

Jinsi ya kufanya; anza kwa kumnong’oneza kwa sauti nzito, kisha libusu sikio lake baada ya hapo unaweza kulamba sehemu ya sikio la nje na baadae kuingiza ulimi ndani ya sikio kabisa. hapa msisimko ni mkali sana na anaweza kukukwepa na kutoa sauti kali ya kimahaba.

3. Ulimi ; ulimi ni sehemu ya mwili ambayo ina mishipa mingi mara mia moja zaidi kuliko ile mishipa ya fahamu ya viganja vyetu. msisimko wa ulimi unasababishwa kumwagika kwa homoni ambazo zinatuletea furaha ya mioyo yetu.

Jinsi ya kufanya; busu tu  inatosha kusisimua ulimi wa mtu wako, bahati mbaya kuna watu hawajui kubusu. ukiwa unabusu mtu usipanue mdomo mzima kama samaki mfu… fungua mdomo wako kidogo kisha nyonya lips za juu wakati mtu wako ananyonya za chini na hii ndio busu linavotakiwa kua.

4. Shingo; hii ni sehemu ya mwili yenye ngozi laini sana ambayo inasisimka hata kwa kuipumulia tu na pua. ni moja ya sehemu nzuri sana kunyonya, kulamba na kubusu.

Jinsi ya kufanya; ukiwa umemkumbatia mtu wako basi busu upande wa kulia au wa kushoto wa shingo huku ukinyonya ngozi la eneo hilo.

5. Chuchu; wanaume wengi wanatumia sehemu hii kama sehemu kuu kumsisimua mwanamke, ni kweli kabisa tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya ubongo ambayo husisimuka chuchu za mwanamke zikiguswa ni sehemu hiyohiyo ambayo inasisimka kinembe na uke vikiguswa. kwa hiyo ni moja ya sehemu muhimu sana.

Jinsi ya kufanya; tomasa matiti yote ya mwanamke kwa kutumia mikono yako miwili kisha nyonya chuchu yake taratibu huku kama unaing’ata na kuiachia. badilisaha kwa kuchocha chuchu ya kulia na kushoto.

6. Kiuno au mgongo wa chini; kama umechunguza ni kwamba wanawake wengi husisimka sana wakiguswa viuno vyao ghafla hata wakati wa kukumbatiwa tu. hii ni sababu ya mishipa ya fahamu inayoenda hadi kwenye sehemu zake nyeti hupita huko.

Jinsi ya kufanya; tomasa kama unafanya masaji sehemu ya chini kabisa ya kiuno kabla makalio hayajaanza. hii itamfanya arelax sana lakini pia kuongeza damu kwenda sehemu zake nyeti tayari kwa tendo la ndoa.

7. Tumbo; tumbo ni sehemu ambayo watu wengi hawaitilii manani sana lakini misuli ya tumbo imeungana na uke moja kwa moja ndio maana baadhi ya wanawake hufika kileleni kwa kufanya mazoezi ya tumbo kitaalamu kama core exercises..

Jinsi ya kufanya; tomasa tumbo lake kwanzia juu kabisa ya tumbo na kwenda tumbo la chini na kisha busu taratibu maeneo mbalimbali ya sehemu ya tumbo na unaweza kumalizia kwa kunyonya kitovu.

8. Katikati ya mapaja; hii ni sehemu yenye msisimuko mkubwa kwenye mwili wa mwanamke, watu wanaondesha magari wanajua siri hii kwani wakimpakia mwanamke wanatumia njia hii kumsisimua kwa kuweka mkono mmoja kwenye mapaja yake.

Jinsi ya kufanya; shikashika sehemu za katikati ya mapaja kwanzia magotini kwenda mpaka karibu na uke.unaweza fanya hivyo wakati ukiwa unambusu.

9. Nyayo za miguu; nyayo za miguu zikiguswa hata kwa mtu ambaye sio wa kike zina msisimko sana kama wa kutekenywa hivi na sina msisimko mkubwa kuliko sehemu nyingi nilizotaja.

Jinsi ya kufanya; shika nyayo moja ya mguu kisha kwa kutumia viganja viwili tomasa katikati ya mguu kwanzia kwenye kisigino mpaka kwenye vidole.usitumie nguvu nyingi…

10. Kinembe [critoris]; hii ni sehemu ya mwanamke ambayo kazi yake ni kuleta msisimko tu na raha kwa mwanamke..eneo hili linazaidi ya mishipa ya fahamu 8000, ni eneo dogo sana lakini shughuli yake sio ndogo. naweza kusema ndio eneo lenye msisimko mkali kuliko yote niliyotaja hapo juu na likiguswa tu mwanamke analoana kabisa.

Jinsi ya kufanya; kidole chako kikubwa cha kinganyani bonyeza na kuachia sehemu hiyo kama mtu anayekagua parachichi pia sugua kwenda chini, juu na pembeni kuangalia muhusika anapenda wapi zaidi pia kama una uhakika na usafi au afya ya muhusika unaweza lamba lwa kuzungusha ulimi sehemu hiyo.

Mwisho; sehemu zote nilizotaja hapo juu ni muhimu sana kwa ajili ya kumuandaa mwanamke japokua kila mwanamke anapata msisimko zaidi kutokana na yeye mwenyewe alivyo yaani mwingine shingo linaweza kua na msisimko wa kawaida likiguswa lakini mwingine ikawa  msisimo mkali zaidi.

JINSI Ya Kumtext Mwanamke Hadi Akupigie Simu Wa Kwanza

Kutumia sms kuanzia wiki hadi mwezi bila kupiga simu ni VIBAYA. Unahatarisha kuitwa boyfriend wa sms, na labda hautakuwa boyfriend wake wa ukweli. Kuondoa hizi athari unapaswa kutumia maujanja haya matatu.Mbinu
#1: Toa majibu yasiyokuwa moja kwa moja.
Wanawake wanapenda majibu ya moja kwa moja kama wanataka kujua kitu flani kutoka kwako. Mwanamke anaweza kukuuliza “Wewe unafanya kazi gani?” ama “Uko na tatoo kwa mwili wako?” Usijibu maswali haya moja kwa moja.
Badala yake mzungushe  kwa kumwambia “Mimi ni jasusi siku za juma halafu wikendi nafanya kazi kwa club kama bausa.” Kama ataudhika na jinsi umekataa kujibu swali lake moja kwa moja, unaweza kumwambia “Nitakwambia tukikutana” ama “Nitakwambia wakati tunaongea kwa simu.”Mbinu
#2: Mtumie meseji ya utani kama hakukujibu.

Kama atashindwa kukutumia meseji baada ya lisaa moja, mwambie “Umefutwa kazi.” Atakupigia na kutaka kujua ni kwa nini umemwambia hivyo na atataka ueleze kwa upana umemaanisha nini.Mbinu #3: Weka ratiba ya kupiga simu.

Kama mnatext na moto, kama vile anareply texts zako chini ya dakika moja baada ya kumtumia text, katiza maongezi yanu kwa kumwambia “Hey, nataka kwenda, lakini nitakupigia simu kesho jioni.” Kama utafanya hivi vile inavyotakikana atataka akupigie wewe simu na atakuwa active wakati wote.Wakati unatimiza mbinu hizi, kuna sheria ambazo unahitajika kufanya ili akuheshimu wakati wote.Sheria
#1:  Moja kwa moja – Anapaswa kutuma angalau jumbe mmoja kwa kila jumbe ambayo utamtumia.Sheria
#2: Kama hatajibu meseji yako moja, usimtumie meseji siku nzima. Kama hatajibu meseji yako ya pili usimtumie jumbe wiki nzima.Sheria #3: Usimtext ukimwambia jinsi unahisi vibaya kwa kuwa anakataa kujibu meseji zako badala yake umpigie simu na umsunze kuhusu simu yake.Waweza kusema “Hi, najua kuna kampuni ambayo itakulipia bili ya wiki nzima ya mjazo wako wa simu kwa kufanya kazi mfano wa mhudumu wa hoteli. Je unataka nikuunganishe?Kwa kutumia mbinu hizi tatu + hizi sheria tatu utakuwa uko sawa katika gemu ya kutext.
NB Mbinu hizi zitafanikiwa kirahisi iwapo umejenga tenshen ya kimapenzi kati yako na mwanamke. Hivyo kama unaanza kumtext mwanamke siku ya kwanza mbinu hii haitafanikiwa.

Linogeshe penzi lako kwa kuzingatia mambo haya !

WAPENZI wasomaji wangu, naomba leo niende moja kwa moja kwenye mada yangu ya wiki hii ambayo kwa kiasi kikubwa inawagusa wanawake. Nazungumzia mambo ambayo mwanamke anatakiwa kuyazingatia ili aweze kumshika ipasavyo mumewe na kuinogesha ndoa yake.

Ni mengi anayostahili kufanya mke kwa mumewe lakini kwa leo nitazungumza machache ambayo naamini yatakuwa na manufaa kwako.

Timiza wajibu wako kama mke
Mwanamke anayemjali mume wake ndiye anayetimiza wajibu, lakini wengi hujikuta wakisalitiwa au kuachwa kabisa na waume zao kutokana na ufahamu mdogo ama dharau ya mambo madogo.

Ni busara kutambua kwamba, ndoa haina mambo madogo. Kila kitu kina umuhimu mkubwa kulingana na nafasi yake sambamba na utekelezaji wako. Mfano, kumpokea bahasha anaporejea kutoka kazini ni kitu kidogo tu ambacho wewe unaweza kukidharau lakini thamani yake kwa mumeo ni kubwa kuliko unavyofikiria.

Tambua kuwa, mwanaume harogwi kwa limbwata la sangoma, mahaba peke yake yanatosha kumshika vilivyo. ‘Ukimhendo’ kwa kiwango kitakachomridhisha, hatawaza kukuacha. Unawezaje? Jibu ni rahisi, muoneshe unampenda na uthibitishe mapenzi yako kwa vitendo na si kwa maneno tu.

Daima hili liwe kwenye akilini yako, mwanamke kupitia mapenzi yake ana uwezo mkubwa mno, lakini lazima awe anajua kutimiza wajibu wake kwenye maisha ya ndoa.

Kama mumeo anakuacha, ujue kuwa kuna mambo unayomkosea na kuyafanya mapenzi yako yageuke kuwa kero kwake. Unyenyekevu kwa wanawake wa kisasa kimekuwa ni kitu adimu sana kiasi ambacho kimekuwa kikihatarisha ndoa zao.

Wanaume wanawapenda wanawake ambao hujionesha waziwazi kuwa wenyewe ni wasaidizi wao wakuu katika masuala mbalimbali. Hawavutiwi na wale ambao hupuuza mambo kwa visingizio visivyokuwa na maana.

Kuwa mjanja kiana
Sababu ya wanaume kuwapenda wanawake wajanja ni kukwepa aibu wanazoweza kuzipata pindi watakapokuwa kwenye uhusiano na wanawake washamba.
Huogopa kujiingiza katika mapenzi na watu wasio na uelewa mpana wa mambo ambao  huwafanya kuwa mafundi wa kuiga mambo yasiyofaa.

Washamba mara nyingi huwa ni malimbukeni, hujifunza mambo yasiyokuwa na faida kwa imani kwamba naye ataonekana mtu kati ya watu. Wanawake wa aina hii ni rahisi kuwaingiza wenzi wao katika hasara kubwa. Hawakawii kusaliti pamoja na kudanganyika kwa mambo madogo.

Wanawake malimbukeni huharibika vibarazani na saluni kutokana na sifa kubwa ya umbeya kwenye sehemu hizo. Wanaume wasiokuwa na subira hujikuta wakiwaacha wake zao mapema, mara tu wanapoanza kuhisi nyendo zisizoeleweka kwa wenzi wao.

Tumekuwa tukishuhudia wanawake malimbukeni wakiiga tabia za ulevi wa pombe, kuwa na makuu katika maisha yao kutokana na kuwaona wenzao wakiwa hivyo. Hili ni tatizo ambalo wewe mke wa mtu unatakiwa kuliepuka ili uishi milele na mumeo.

Siku zote mwanamke mjanja hawezi kuiga hovyo hovyo, siku zote anajua kitu cha kuanzia na kinachofuata. Hadanganyiki kirahisi na hiyo ni sifa kubwa ambayo inaweza kuinogesha ndoa yako kwa kiasi kikubwa.

Jinsi ya kumfanya mumeo awahi kurudi nyumbani

Inawezekana ukawa upo kwenye mahusiano yenye changamoto ya Mume wako kuchelewa kurudi nyumbani, Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kukusaidia kumrejesha mapema nyumbani.

Jambo la kwanza ni vizuri ukajiuliza kama kweli upo katika ndoa sahihi, kwa kutizama chanzo cha mahusiano yenu ni kitu gani kilichowaunganisha lakini Pia ukajiuliza bila kujidanganya wewe na Mumeo mnafahamu maana halisi ya mapenzi ?

Baada ya maswali hayo naomba ufahamu kwamba mapenzi yoyote yale lengo lake kubwa ni kuleta utulivu na kuhurumiana.

Je ndoa yako inakupa utulivu na mnahurumiana?, kama mnahurumiana iweje Mumeo achelewe kurudi nyumbani huku akijua fika kwamba wewe Mkewe hupendi achelewe kurudi nyumbani na kuchelewa kwake kunakuondolea utulivu ?.

Hatua Zifuatazo zitakusaidia kumrejesha Mumeo nyumbani mapema:

  • Je wewe sio chanzo cha Mumeo kuchelewa kurudi nyumbani? Na kama wewe unachangia kwa namna yeyote ile basi rekebisha yale asiyoyapenda Mumeo na hapo utakuwa umemaliza tatizo. 
  • Pambana na tatizo na sio Mtu, tambua tatizo, tafuta elimu ya tatizo husika ili upande daraja. 
  • Kuwa mvumilivu, mwenye hekima, busara, msikivu, mwenye kusamehe na kusahau. 
  • Kiri makosa yako na omba msamaha. 
  • Kubali kushindwa na usiwe mshindi kila siku hata kama umeshinda. 
  • Penda kabla hujapendwa. 
  • Toa kabla hujapokea. 
  • Japo inauma lakini usimuulize alikuwa wapi na kwa nini amechelewa kurudi. 
  • Mkaribishe kwa bashasha na mpe pole ya huko alikotoka. 
  • Hakikisha anakukuta ukiwa msafi na mwenye mvuto kama vile umerudi kutoka matembezi. 
  • Mpe chakula na kaa ule pamoja nae na kama ulishakula kaa karibu yake. 
  • Onesha kama vile unafurahia yeye kuchelewa kurudi, japo unaumia kwa ndani. 
  • Usioneshe kama vile una wivu wa yeye kuchelewa kurudi, bali onesha kuwa unahofia usalama wake anapochelewa kurudi. 
  • Usimnyime tendo la ndoa hata kama kachelewa kurudi na furahia tendo hilo kama vile ulikuwa ukimsubiria kwa hamu. 
  • Anapotoka onesha kama vile na wewe utatoka lakini usitoke bila ridhaa yake.

Tambua Jinsi Ya Kuongeza Mvuto Kwa Mpenzi Wako

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia.

Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine.

Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Kanuni kumi ’10’ za kuwa mke mwema

UHALISI WA MAISHA:
Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo;

UVUMILIVU:
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

UPENDO WA DHATI:
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia.

UTII KWA KWA JAMII:
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka  ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii  kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.

UAMINIFU KATIKA JAMII:
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote.
UNYENYEKEVU WA KWELI:
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.

UWAJIBIKAJI WA DHATI:
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

USHIRIKIANO WA DHATI:
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora.
UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO:
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.
KUFANYA TATHIMINI:
Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati.

MAMBO YA KUZINGATIA IWAPO UNATAKA KUSHIKA MIMBA

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini. Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo.

Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokeo kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindindwa kubeba mimba.

Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au ‘couples’ 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba.

Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.

Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…

• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamona dokta wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na

1. General examination au uchunguzi wa jumla.

2. Kipimo cha kensa au Pap smear.

3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambao wanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.

4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.

5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.

6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyuma (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.

7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-

• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.

• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo ‘stress’ huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.

• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)

• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:

• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.

• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.

• Jiepushe kunywa kahawa na binywaji vinginevyo venye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.

• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.

• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri.

Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.

• Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa.

Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanamme wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo. Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia. Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na

matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanamume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshe kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.

• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

Tahadhari Kwa Wadada Mnaopenda Kuvaa Shanga Kiunoni…

Bwana Yesu asifiwe!!!

Wanawake wengi wanapenda kuvaa shanga kiunoni wakiamini zinawavutia wanaume wengi katika mapenzi.Napenda kutoa tahadhali kwa wanaopenda kuzivaa hasa kiunoni kuwa asilimia 80% ya shanga zinazouzwa zikiwa zimeshasokotwa zinatengenezwa na waganga WA kienyeji au watu ambao ni mawakala WA shetani na kuzinuizia mapepo kwa malengo yafuatayo:

Kuharibu au kuiba nyota za watu
Kuwafunga wanawake uzazi
Kuwaunganisha na mtandao WA kuzimu
Kuvuruga mfumo WA hedhi WA wanawake
Kuwafanya wanawake kuwa makahaba, kwa sbb unatamani kukutana na wanaume wengi ili wakujue km unavaa shanga na unazitumia
Kuwafunga kimafanikio
Kuwafanya wasidumu kwny ndoa wanapoolewa.
Kuwafanya wafikirie ngono zaidi.

Sasa unaweza usinunue kwa mganga lakn aliyetengeneza ni mganga au agent WA shetani.

Ww unaweza kununua kwa MTU na ukamwona WA kawaida, au yeye anaeuza yamkini hajui lakn alyetengeneza alikuwa na kusudi.

Unahitaji kuwa makini sana Dada zangu na vitu vinavyovaliwa sirini.

Ni unaponunua ukazikomboa kwa damu ya Yesu ili kufuta Yale maagano na manuizo yalyoambatanishwa nayo.

Sio kwamba hana hisia, Unasababisha asikutake.

Kwa mwanamke mapenzi ni hisia, hisia za yeye kukuwaza wewe, hisia ya kutaka kukuona kwa sababu hajakuona na anatamani kukuona, hisia ya yeye kuwa na wasiwasi kuhusu mpenzi wake, ukiondoa hicho kitu cha kumfanya akuwaze, basi muda si muda utaanza kumtoka kichwani.

Kuna sehemu kwenye maisha mwanaume kama mwanaume inabidi uwe mwanaume, ujitenganishe kati ya hisia unazojisikia, uweke utofauti kati ya kile kifurushi ulichonacho cha muanguko wa kihisia na ukweli uliopo, ufanye maamuzi sio kwa sababu ya upendo ila kwa sababu ya kutengeneza mazingira ya kiuhalisia kwa mapenzi ulionayo kwa msichana wako.

Kuachana na maamuzi ya presha ambayo moyo huyafanya kwa uwoga wa kumpoteza mpenzi wako, kwa kuhisi mapenzi kwa mpenzi wako yatapungua na kujikuta unafanya kitu ambacho badala ya kuyaweka mapenzi yako na yule umpendae pazuri, yanakufanya uonekane fala na mtu usiekuwa na maamuzi ya msingi na unayepaparuka kwa kuendeshwa nahisia kiasi cha kumfanya msichana wako haisi utofauti juu yako, kwake unakuona unafanya mambo kupitiliza, kiasi cha kuzidi mipaka unaanza kuboa.

Kwa historia na ufahamu, tokea uumbaji wa binadam, mabadiliko ya kibinadam hutokea sababu tu, binadam hubadilika kwa kuangalia mazingira aliopo, sio sababu tu anakurupuka kufanya kitu ili kutimiza mazingira yanavyoitaji, kwa mfano mwingine ua likisinyaa sio kufanya juhudi la kulifanya lisisinyae ila ni kufanya maamuzi ya kulibadilishia mazingira kama udongo na mbolea ili lichanue.

Hata mahusiano ni hivyo, mambo sikuzote lazima yabadilike, zile stori za kupendana sana ipo siku lazima zitaanza kufifia, na ule ukaribu wa kila dakika kutumiana sms ya “Nakumisi”, utabadilika utakuwa wa saa au kwa siku nzingine utakuwa mara moja kwa siku au kutokuwepo kabisa.

Utofauti huu ukianza na ukaanza kuhisia umbali kati yako na msichana wako unaanza kutokea, sio ndo ufikie maamuzi ya kukurupuka na kupagawa, badala ya kuonyesha upendo uliokua nao wa kawaida unaanza kuingiza shauku na kujipa mawazo na wasiwasi ya kuwa upendo wake umepungua, hivyo kwa asilimia kubwa sana kutokana na wasi wako unaanza kuingiza maamuzi ya kuongeza zaidi kiasi cha kumpenda bila wewe kujijua, unajikuta wewe ndo unaanza kupiga simu zaidi kuliko yeye, unaanza kumtumia meseji zaidi hata kabla hajajibu umesha tuma meseji tano.

Unayafanya mapenzi kuanza kuwa ya upande mmoja kwa kutompa pumzi ya kupumua msichana wako, na kusababisha zile hisia alizonazo kwako kuanza kupungua maana unafanya mambo mengi kwake, japo wewe unaona kawaida ila kwake unaanza kumboa maana hata ule mda wa kumfanya yeye akumisi anakua hana tena, ule muda wa kumfanya yeye akuone kimya na kuanza kukuwaza “Hivi anafanya nini sasa hivi, mbona yupo kimya?” anakuwa hana tena maana kila muda wewe unakuwa unammwagikia kwa meseji na simu mpaka anaanza kusahau hisia zake mwenyewe kwako.

Kwa mwanamke mapenzi ni hisia, hisia za yeye kukuwaza wewe, hisia ya kutaka kukuona kwa sababu hajakuona na anatamani kukuona, hisia ya yeye kuwa na wasiwasi kuhusu mpenzi wake, ukiondoa hicho kitu cha kumfanya akuwaze, basi muda si muda utaanza kumtoka kichwani.

Mazoea ya wewe kuwa ndo unamtumia meseji yeye tu kila saa na kila wakati, kutamfanya yeye asiwe anakutumia maana anajua na kutarajia baada ya dakika kadhaa lazima mlio wa sms yako atausikia, hivyo ile hali ya yeye kukuweka kipaumbele inakwisha kwake, na sio sababu

anataka iwe hivyo bali wewe ndie unaesababisha, kama ujuavyo “demu akikufata fata na kukusonga kwa kila jambo, hata kama unampenda itafikia kipindi ataanza kukuboa na thamani yake kushuka”, basi hicho pia hutokea upande wa pili wa shilingi iwapo tukiwafatilia kupita kiasi na kutojiamini kwa kuwa wanaume dhabiti..

Baadhi ya Mbinu za Kumridhisha mwanaume wako kimapenzi

Heshima kwenu wakuu,

Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!

Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Pamoja na Kumheshimu, sheria zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.

1 Vaa vizuri. 
Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako. Sio unavaa vizuri tu ukiwa unaenda sokoni na kwenye ibada tu lakini nyumbani unajisahau

2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. 
Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali. Sio akikuambia fanya hivi, unaanza eti hizo style za kwa wanawake wako usiniletee, akikuambia fanya hivi eti sitaki, kwanza niache nmechoka. hatakujibu kwa maneno bali vitendo

3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. 
Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, sio dakika mbili tu unahemaa..!! kiasi kwamba unashindwa hadi kuendesha farasi.

4 Kuwa Mchokozi. 
Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake. mkonyeze, mtege, usiogope kumpapasa. ringaringa, jidekeshe.

5 Jiamini na Jipende. 
Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako. sip ooh zima taa, sijui usiniangalie mambo kibao. Tambua hadi amekupende kashakuvua nguo kitambo sana hata kabla hujavua. Inamaana hadi mnaingia chumbani kashakukubali.

Samahani lakini..

Design a site like this with WordPress.com
Get started