ACHANA NA UBIZE USIO NA MAANA, TENGA MUDA WA KUWA NAYE

NI Ijumaa nyingine tu­napokutana katika uwanja wetu huu mzu­ri, tukijuzana na kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali ya­husuyo mapenzi. Mada yetu ya leo ni kama inavyojieleza hapo juu.

Je, mara ya mwisho kwa wewe na mpenzi wako kupata muda wa kukaa pamoja au kutoka ‘out’ ilikuwa ni lini? Una desturi ya kutoka na umpendaye, mkaenda mahali tulivu ambapo mtapata muda wa kujadiliana na kubadil­ishana mawazo kuhusu maisha na mapenzi? Kama jibu lako ni hapana, unaishi kwenye mapen­zi yaliyokosa uhai.

Maisha yanaenda kasi sana, wanandoa wengi au watu am­bao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, wanajikuta wakikosa kabisa nafasi ya kuwa pamoja kutokana na kila mmoja kuweka kipaumbele katika kazi, biashara au shughuli nyingine za utafutaji pesa au malezi ya watoto.

Matokeo yake, watu wengi wanaishi kwa mazoea tu lakini katika uhalisia, mapenzi yana­kuwa yamepungua sana au hayapo kabisa.

Watafiti wa mapenzi wanaeleza kwamba hakuna kazi ngumu kama kuishi pamoja wewe na mpenzi wako, iwe ni kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida wa kimapenzi kwani ni rahisi sana watu kuchokana. Hata kama unampenda vipi, lazima kuna muda utamchoka au utachoshwa na mazin­gira ambayo mmekuwa mkiishi siku zote.

Unapofikia hatua hii, kitu pekee kinachoweza ku-refresh akili na hisia zako, ni wewe na umpen­daye kutoka pamoja na kwenda sehemu tofauti kama ufukweni, hotelini au sehemu yoyote tulivu ambayo mtakaa pamoja, mtakunywa au kula na kufurahi. Kitendo hiki kinata­jwa kuwa siri kuu ya kufufua mapenzi na kuondoa ile hali ya kuchokana.

Haijalishi umeishi kwa muda gani na mpenzi wako, hata kama mna miaka kibao, lazima muendelee kutoana out mara kwa mara. Hata kama tayari mmeshazaa watoto na wamekuwa wakubwa, suala la out halikwepeki kama mnataka kuishi kwa amani na upendo. Wengi wanaamini kwamba mpenzi mpya pekee ndiye anayetakiwa kutolewa ‘out’, jambo ambalo siyo sahihi.

Mkirudi, kila mmoja atashangaa kwamba mapenzi yake kwa mwen­zake, yatazidi ma­radufu, kama kulikuwa na migogoro ya hapa na pale, itaisha na mtaen­delea kuishi kwa amani na furaha.

Wengi tu­nasumbuliwa na kasumba kwamba ili kumtoa mpenzi wako out, ni lazima waleti yako iwe imejaa, lazima mkatumie fedha nyingi au lazima umpe­leke sehemu ya gharama. La hasha, siyo lazima kabisa.

Kwa mfano, inakugharimu nini wewe na mpenzi wako kutoka na kwenda ufuk­weni, mkaagiza soda, maji au vinywaji mnavyovipenda, mkakaa kwenye mchanga wa bahari na kupunga up­epo mwanana?

Hata kama hakuna ufukwe hapo mnapoishi, mnaweza kutoka na kwenda sehemu yoyote tulivu, iwe ni kwenye uwanja wa mpira muda ambao hakuna watu, sehemu za milimani au mahali popote ambapo mtakuwa wawili tu, inatosha kabisa. Unaweza kununua matunda, vinywaji au vitafunwa mnavyovipenda, mkaenda navyo mpaka sehemu mliyoichagua, siyo lazima uwe na fedha nyingi.

Ili mtoko wako na umpen­daye ukamilike, kuchagua sehemu ya kwenda ni jam­bo la kwanza lakini kubwa zaidi, lazima ujue kwamba mkiwa ‘out’, unapaswa kufanya nini ili mpenzi wako afurahi na kufufua upya hisia za mapenzi ndani ya moyo wake.

Ni matumaini yangu kwamba utakuwa umejifun­za kitu kikubwa na nakuhak­ikishia kwamba ukiyafanyia kazi haya, utayafurahia mapenzi.

Enyi Wanaume Ishini na Wake Zenu Kwa AKILI” La Sivyo Mwanamke Atakukoroga Maisha Yako Yote

BIBLIA ILIPOSEMA “Enyi Wanaume Ishini na wake zenu kwa AKILI” Mungu alikuwa anajua anachosema.Kama huna akili Mwanamke atakukoroga maisha yako yote na utaishia kusema “Women are so Complicated”
Wanawake huwa wanaongea vitu ‘Kirahisi-rahisi tu’ lakini huwa vinamaanisha ‘Vitu Vigumu Ajabu’
Wanawake wanaweza kukwambia “Mi nataka Mwanaume anipende tu BHAASSS!!Ukidhani kwamba Upendo wako unatosha kwake UTAKUWA UMEFELI
Wanawake wanahitaji vitu 4 na vyote VIENDE KWA PAMOJA(Perpendicularly),vitu hivyo ni

1.HELA 2.GOOD SEX 3.CARING MAN 4.MUDA
Kuna Wanaume wanajua “Kukaza vizuri” mwanamke anatosheka,na wana hela ila WAKO BUSY…Hii factor ya wewe kuwa Busy tu itamfanya mtu mwingine mwenye Muda “Amkaze kiulaini kabisa” halafu wewe utashangaa…”Mke wangu nampa kila kitu,hela za kila kitu nampa..YES,Amekaa muda mrefu uko bize unasaka hela na adui namba 1 wa Mwanamke ni LONELINESS….
A lonely Woman can easily be trapped by anyone..hata Houseboy akimpa ATTENTION endlessly anakula mzigo
Unataka Mwanamke awe wako peke yako???Fuata kanuni ya KIBIBLIA, ishi nae kwa akili….Mpe MUDA..Mpe HELA…Mpe Kisago kitandani…Mpe CARE na ATTENTION
Sikiliza maneno ya Nabii Seth uyatendee kazi,maana TB JOSHUA hatakwambia haya KAMWE!Nimemaliza!

Yafahamu mambo ambayo ni sumu katika mahusiano yako na mpenzi

Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi.

Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi.

1. Wivu kupindukia.

Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi.

Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.
2. Kutompa nafasi mpenzi wako.

Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi.

Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha.
3. Kumuingilia mpenzi katika mambo yako.

Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.

Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako.

Makosa Wanayofanya WANAUME Walio Kwenye Ndoa

  1. Kuja na vimada mpk home na kumuacha ndani ya gari
  2. Kuingia ndani na viatu vya matope wakati kumeshadekiwa
  3. Kuvurugua nguo au vitu wakati wa kutafuta kitu kabla ya kuuliza kilipo.
  4. Kumtambulisha mtoto wako kwa kimada wako.
  5. Kumleta rafiki yake kuja kula bila kutoa taarifa.
  6. Kumsifia rafiki au ndugu wa mke wa kike kuwa anavutia bila hofu.
  7. Kukosoa muonekano wa mke bila kujali atajisikiaje.
  8. Kutosema chochote mke akipendeza mpaka aulize.
  9. Kujifutia taulo na kuliacha ovyo bila kulianika
  10. Kutotandika bed mke asafiripo na kugeuza bed kama kiota cha ndege
  11. Kutofua boxer na socks zake hadi wife awepo na kama kasafiri zitasubiri arudi

MPENZI WAKO ANAKUFANYIA KISIRANI BILA SABABU? SOMA HAPA

KWA watu waliopo katika uhusiano wa kudumu, watakubaliana na mimi kwamba kuna wakati huwa inatokea mwenzi wako anaamua tu kukufanyia kisirani, na hii inawahusu zaidi wanawake, hataki kuzungumza chochote na wewe.

Kila unachomuuliza anakujibu kwa mkato kisha anaendelea na mambo yake, hataki kushirikiana chochote na wewe na hata haki yako ya msingi huipati!

Wengine huweza kudumu kwenye hali hii kwa muda mrefu na kama usipokuwa makini, hii inaweza kuwa sababu itakayowaingiza kwenye matatizo makubwa zaidi. Bahati mbaya ni kwamba, ni wanaume wachache sana wanaoelewa nini cha kufanya inapotokea mwanamke unayeishi naye, au unayempenda sana anakubadilikia kiasi hiki.

Yaani unamuona kabisa hayupo sawa, hakuchangamkii, hataki kuzungumza na wewe lakini unapomuuliza kama ana tatizo lolote, anakujibu kwamba hakuna tatizo lolote na yupo sawa.

Wengine hudhani kwamba mwanamke husika ameanza dharau, amepata wanaume wanaompa jeuri au hampendi tena! Kama nilivyosema, ukishindwa kujua hali yake imesababishwa na nini na unatakiwa kufanya nini ili kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida, unaweza kujikuta ukisababisha matatizo makubwa zaidi.

Kwa hiyo, jambo la msingi unatakiwa kuwa mwepesi kumsoma mwenzi wako na hii itakusaidia kumgundua muda ambao hayupo sawa. Ukishagundua kama hayupo sawa na anakuwekea mgomo baridi, muulize kwa upole kama yupo sawa au kama kuna kitu kinamsumbua. Bila shaka majibu yake yatakuwa ni yaleyale, ‘nipo sawa’, ‘hakuna tatizo’ na mengine ya aina hiyo.

Ukisha muuliza mara moja au mbili akakujibu vilevile, huna haja ya kuendelea kumuuliza mara nyingi zaidi kwani utasababisha azidi kukasirika. Kwa jinsi tulivyoumbwa, wanawake wanaongozwa zaidi na hisia.

Unapomuudhi mwanamke wako jambo fulani, kitu pekee anachoweza kukifanya kukuonesha kwamba amekasirika, ni kukulalamikia lakini akiona huelewi au kama humpi nafasi ya kulalamika, basi huishia kukununia.

Kwa hiyo unapoona amefika katika hali kama hiyo, tambua kwamba kuna ujumbe anataka kukufikishia! Anataka kukuonesha kwamba umemkasirisha, umemuumiza moyo wake na hafurahishwi na matendo yako.

Unachotakiwa kufanya kwanza ni kutulia lakini pili ni kuanza kujichunguza mwenyewe, ni jambo gani umefanya mpaka ukamuudhi? Jiulize mwenyewe ndani ya kichwa chako lakini wakati huohuo, tambua kwamba anahitaji sana ‘attention’ yako. Mwanamke akinuna, anataka umuoneshe kwamba umeshaelewa kwamba hayupo sawa
na unajitahidi kumfanya arudi kuwa sawa! Wengine wanakosea hapa, akishaona amenuniwa, basi na yeye anaanza visa, anaanza kufokafoka na kuwa mkali, hayo ni makosa.

Unatakiwa kushuka chini hata kama bado hujajua kosa lako ni lipi, kuwa mpole kwake, muoneshe kumjali, jitahidi kujiweka karibu naye na mfanyie mambo mazuri.

Kama unajiweza, unaweza hata kumuomba mtoke ‘out’, kama amekasirika sana anaweza hata kukataa kutoka na wewe lakini ni jukumu lako kumbembeleza. Kihulka wanawake wameumbwa kubembelezwa kwa hiyo katika mazingira kama hayo ni nafasi yako ya kuonesha uwezo wako wa kumbembeleza mpaka akubaliane na kile unachokitaka.

Ukishapata nafasi ya kutoka naye, au hata kama hamjatoka mpo wenyewe mahali tulivu, anza kuzungumza naye kwa upole ukitanguliza maneno matamu ya kujishusha na kumuomba akusamehe, bila shaka kama kuna jambo umemuudhi atakueleza kwa uwazi, hata kama unaona siyo jambo la msingi sana, rudia ukamuombe radhi na mhakikishie kwamba hautarudia.

Utashangaa anaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na lile tabasamu lililopotea kwenye uso wake litaanza kuchanua upya. Ukitumia nguvu na ubabe, utakuwa sawa na mtu anayemwagia petroli kwenye moto. Kwa leo ni hayo tu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

HATA KAMA HUMWAMINI, MPE UHURU WAKE

NI SIKU nyingine tunapokutana, ni wajibu wetu kumshukuru Mungu kwa kutufanya tuione siku ya leo. Leo ningependa kuzungumza na wewe msomaji wangu mwenye tabia ya kumbana mwenzi wako mpaka anahisi kero. Wivu ndiyo mapenzi, hilo halina shaka lakini kila kitu kinapaswa kuwa na kiasi.

Kuna watu wanaamini kwamba eti mpenzi wako, awe mwanaume au mwanamke, ukimbana sana ndiyo hawezi kukusaliti. Kwamba muda wote lazima uwe unajua yuko wapi, anafanya nini na lazima atoe ushahidi wa kila ana­chokifanya kwako. Huko ni kujidanganya, mtu mwenye tabia ya usaliti, hata ufanye nini bado atakusaliti tu. Unachopaswa kukijua, ni kwamba hakuna kitu muhimu maishani kama kumpa uhuru mwenzi wako.

Najua inaweza kuwa ngumu kwako kuelewa ninachokisema kama umezoea ‘kukaba mpaka penalti’. Ni vizuri kufahamu nyendo za mwenzi wako na kuwa na taarifa juu ya kila anachoki­fanya lakini narudia kusisitiza, ni muhimu kumpa uhuru wa kutosha.

Kwa kawaida, kila mtu kuna wakati huwa anatamani uhuru wa kufanya mambo yake binafsi, hii haijalishi mtu yupo ndani ya ndoa au laah! Upo muda ana­tamani kukutana na rafiki zake waliosoma pamoja au waliokua pamoja, upo muda anahitaji kuji­kumbusha enzi zake na mambo kama hayo. Sasa kama wewe unatanguliza wivu kwa kila anachokifanya, hutaweza kumpa uhuru wake.

Utambana kwa kila namna, hata atakapokuomba ruhusa lazima utamnyima, matokeo yake, moyo wake utaingiwa na sononeko na mambo yakiendelea hivyo, taratibu ataanza kujenga chuki na wewe.

Mkiendelea hivyo kwa muda, mtajikuta ufa mkubwa umeanza kujengeka kati yenu. Mwache huru, na kama wasiwasi wako ni kwamba atakusaliti, hata ukim­bana bado anaweza kukusaliti pia. Tena muda mwingine, usisubiri akuombe, kuonesha kwamba unamjali mruhusu aende kutembea sehemu yoyote anayoipenda akiwa peke yake au na rafiki zake, ikiwezekana mpe hata fedha za matumizi kwenye matembezi yake.

Kama mna watoto, unaweza kuamua kubaki na watoto ili apate ule uhuru wa kuwa mwenyewe kwa sababu akiwa na watoto hawezi kuwa huru kwa asilimia 100. Wazee wa zamani, walikuwa na kawaida kwamba, akikaa na mkewe kwa muda fulani, anam­ruhusu aende nyumbani kwao kusalimia.

Anaweza kukaa kwa siku kadhaa na akiwa huko hamfuatilii kwa jambo lolote zaidi ya kuhakikisha yupo salama. Wapo ambao mpaka sasa huwa wanafanya hivyo na wataalamu wa saikolojia ya mapenzi, wa­naielezea mbinu hiyo kama njia nzuri ya kuimarisha hisia za mapenzi kati yako na umpendaye.

Mwanamke wa aina hiyo, akipata uhuru wa kwenda kwao ambao tafsiri yake ni uhuru wa kuwa mwenyewe, akirejea huwa na hisia mpya kabisa za mapenzi na hata kama kulikuwa na visasi na vinyongo ndani ya moyo wake kwa sababu ya jambo ambalo mmewahi kukwazana, vyote huisha na kuanzisha ukurasa mpya kabisa.

Sasa ukiangalia kwa kina, hiyo haina tofauti na uhuru ninaouzungumzia hapa, kama hana sehemu ya kwenda akakaa siku kadhaa, basi msaidie kwa kuwa unampa uhuru wa kuwa mwenyewe mara kwa mara. Alikupenda akiwa mwenyewe na ili aendelee kukupenda, lazima uwe unampa muda wa kuwa mwenyewe. Kwa leo ni hayo tu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

Kina Kaka Acheni Ujinga, Hakuna Mwanamke Asiyetaka Kuhongwa! Shauri Lako

Wakaka acheni ujinga, ukitaka dem wa peke yako basi jua kugharamia. Nakwambia wanawake asilimia kubwa hukumbuka fadhila za mtu anayemgharamikia kuliko wanaume wa ai lavii yuu maneno.

Usidanganyike hakuna mwanamke asiyependa kuhongwa, kuna wanawake natural hawawezi kuomba,ila anakua anataka ujiongeze, sasa kama wewe ni wale ambao akikwambia “baby kifurushi kimekata” unajibu “basi mumy pls ukiweka nicheki” umekwishaaaa!!!

Anakueleza shida zake unasema “mpenz vumilia nakuombea upate kazi” kaka umeishaaa kabisaaaa aiseeee!!! Huna chako!!!
Ujue ulivyokata simu umefatiwa na bonge la msonyoooo ka sio tusi la nguoni basi la mwilini. Yani wewe kama ni wale wa baby mwezi huu mambo yangu hayako sawa, nakuapia unagongewa weeeeeeeeee . . . . mpaka ujute!!

Unamuona dem wako kasuka, kapendeza na hana kazi, we umekazana tu “beibi umependeza” . . . . . . Yaani wee boya ujue!! Mume mwenzio kaweka nguvu, so anapokua anatoa calendar za kukuona tulizana, service inakua kwa anayehudumia.
Hakuna dem wa siku hizi anayetaka kuambiwa nakupenda jumapili mpaka jumapili we mhonge tu uone heshima.

Jinsi ya Kuepuka Vizinga vya Mwanamke

Siyo ajabu kumsikia mwingine akisema; “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nitakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri, maisha yanaendelea. Yaani ni full kujiachia.”

Si hivyo tu, wapo wanaume ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.

Unaweza kumsikia mwanaume akisema; “Aaah! Yule demu kazimika ile mbaya na mapigo yangu, kila ninachotaka ananinpa anajua akinizingua namtosa, hadi mshahara wake akipata ananigawia. Yule ndiyo mwanamke wa kuwa naye bwana!”

Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na pesa, ukiona mpenzi wako anaweka pesa mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze kwamba huna kisha muangalie jinsi gani mnaweza kusaidiana katika kutatua tatizo linalomkabili.

Itakuwa sio busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona kwamba unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana, na hili ni kwa pande zote mbili.

Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ?out?, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au hana. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka?

Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu nani? Fanya mabadiliko tafadhali. Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba pesa kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo sio ya msingi, vipengele vifuatavyo vinafaa sana kwako…

MWELEZE UKWELI
Kama huna pesa wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ?mizinga? ili afaidi.

Ishi kawaida, kuwa mkweli kwake siku zote, utakapokuwa mkweli kwake atakuheshimu kwa uwazi wako. Siku zote zilingane, uwe una fedha au huna asijue, hilo litakusaidia kwa kiwango kikubwa sana katika maisha yako ya kimapenzi.

JENGA MAZINGIRA YA YEYE KUKUSAIDIA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa! Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya daladala analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.

BANA MATUMIZI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo! Wakati akiwa anaamini hivyo, ukweli ulionao moyoni ni kwamba huna fedha za kutosha.

Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakusababishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

Kwa kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku moja na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga ‘mizinga’ mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.

Mambo yanayochangia Upungufu wa nguvu za kiume

LEO ninataka tuangalie kwa kina mambo yanayochangia tatizo hilo upungufu wa nguvu za kiume. Ningependa tulio katika ndoa, ukishaisoma makala hii tuwahusisishe wenza wetu nyumbani au mpigie rafiki yako na kumueleza kuwa ana nafasi ya kujilinda kupoteza
nguvu za kiume na hivyo kuwa na uhakika wa amani nyumbani.
Nasema amani kwa sababu tatizo hili huingilia amani nyumbani kwani kuna kuhisiwa kuwa mwanaume anajihusisha na nyumba ndogo maarufu. Uzoefu katika vituo vyetu vya Marie

Stopes kina mama ndio huja kutafuta ushauri kwa nini mzee kabadilika na wafanye nini ili kumrudisha nyumbani. Zifuatazo ni sababu amabazo kitaalamu zinatajwa kuchangia kupungua kwa nguvu za kiume na nyingi kama si zote zinaepukika.

Msongo wa mawazo: Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale

watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

5. Umri: Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu

nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo

MAMBO 2 MUHIMU YA KUMFANYIA MPENZI WAKO PINDI MNAPO MALIZA KUFANYA MAPENZI.

Wanaume na wanawake walio wengi pindi wanapomaliza kufanya mambo yao na wapenzi wao chumbani hujikuta wakikaa pembeni bila kuzingatia vitu muhimu vinavyotakiwa kufanywa pindi wanapomaliza kusex.

VIFUATAVYO NI VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA PINDI UNAPOMALIZA TENDO NA MPENZI WAKO CHUMBANI:
1. MFUTE FUTE MPENZI WAKO – Mpenzi msomaji faham kuwa unapokwenda kufanya mapenzi na mpenzi wako hakikisha unakwenda ukiwa na kitambaa kisafi (LESO) hiki kitambaa unakuwa nacho maalum kwa ajili ya kumfuta mpenzi wako pindi mnapomaliza kufanya mapenzi. Hakikisha unapomaliza kusex na mpenzi wako unamfuta jasho mwilini na pitisha kitambaa chako katika sehemu zake za siri mfute fute taratibu mpenzi wako usikubali mpenzi wako ajifute yeye mwenyewe na usisubiri akuambie umfute.

2. MUULIZE MPENZI WAKO KAMA KARIDHIKA AU BADO ANAHITAJI KUENDELEA: – Wapenzi waliowengi wanapomaliza kufanya mapenzi huwa hawaulizani swali kama hili wengi hujistukia na kuamua kuvaa nguo zao na kuondoka hili ni kosa kubwa, siku zote katika mapenzi mwanaume huwah kufika kileleni kuliko mwanamke hivyo mwanaume hujikuta ameisharidhika ikiwa mwanamke hajaridhika hivyo nivizuri pindi unapojiona umeridhika muulize na mpenzi wako kama nae

karidhika akikuambia tayari basi mnaweza kuishia hapo au akikwambia bado ni wajibu wako wewe kuendelea tena kufanya mapenzi mpaka nayeye aridhike. Lakini kunatatizo moja hujitokeza sana kwa upande wa wanawake wanawake walio wengi wanapoulizwa na wapenzi wao kama wameridhika huwajibu wapenzi wao “Ndio nimeridhika” lakini kumbe bado hawajaridhika. Napenda niwaambie wanawake wote wenye mtindo huu kuwa si mzuri kuweni wakweli pindi unapoona hujaridhika usimfiche mpenzi wako mwambie ukweli kwani ni haki yako kuridhishwa.

Design a site like this with WordPress.com
Get started