MANENO YA MAHABA KWA MPENZI WAKO….

leo nataka kuzungumzia maneno ya mahaba, jamani tunajuwa ya kwamba ukiwa na mpenzi wako unafurahi zaidi pale japo muda fulani atakupa maneno matamu, na mazuri na yenye kuzidi kukupa moyo wa wewe kuzidi kutaka kuwa naye…

sasa kuna wapenzi wengine hata mimi nilishapitia mmoja wakati fulani, jamani wanaume na wanawake wenzangu hebu tujitahidi maneno kama mpenzi, honey, sweety, mkiwa mbele za watu kumuita mpenzi wako sio mbaya maana wengine haswa waliozaa utasikia baba fulani mara mama fulani inamaana baada ya kuzaa mpenzi, sweety, honey umeisha?????? tunawapenda sana watoto wetu lakini wao wananafasi yao na mwenza wako ananafasi yake…

kwenye sita kwa sita watu utawakuta kimya tu madai wanasikilizia uhondo, jamani kuna maneno pale ama mnaoneana aibu sasa kwangu raha mpenzi aongee aniambie anavyojisikia wapi niongeze, vipi nikae, wapi nimshike kwa sauti ya taratibu na yenye mapenzi tele….sijui wewe mwenzangu

sasa pakiwa kimya tu jamani na ndio kwa mfano kitanda ndio vileeee ukigeuka tu majirani mpaka watujuwa hizo kwinyo kwinyo kwinyo hapo kwenye mechi sindio balaa maana utakuwa usikilizii raha unakilaani kitanda tu hichi nacho mpaka watu wajuwe leo napewa…..

kama mnaona aibu kuongea basi kama chumbani kuna redio wekeni hata mziki wa taratibu kuwahamasisha zaidi, maana ule ndio utakaoongea kwa niaba…

maneno ya mahaba jamani ndio mafuta tosha ya kuendesha hilo gari la mapenzi.

ATHARI ZA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI KWENYE TENDO LA NDOA

TATIZO hili la mwanamke kutofikishwa kileleni wakati wa kujamiiana huitwa ‘Female Orgasmic Disorders’ kufika kileleni tunaita ‘orgasm’ au ‘climax’.
Kila mwanamke ni lazima afike kileleni wakati wa tendo hili.Hii ni hali ya kimaumbile ambayo imeumbwa na Mungu.


Mwanamke hufika kileleni pale anapokuwa amesisimka kwa kiwango cha hali ya juu. Hali ya msisimko kwa mwanamke tunaita ‘sexual arousal’ na huanzaia pale mwanamke anapokuwa na hamu ya tendo hili la kujamiiana yaani ‘sixual desire’.Kwa kawaida msisimko hukolezwa wakati wa maandalizi ya tendo au ‘romance’ kwa kutumia milango mitano ya fahamu.Kila mwanamke ana jinsi yake ya kusisimka wakati huu wa maandalizi kutegemea na aina ya mlango wa fahamu unaomsukuma, mfano kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa. Wapo wanawake wanaosisimka na mlango mmoja, wengine miwili au zaidi.


MAANA YA KUFIKA KILELENI
Tunaposema mwanamke au mwanaume amefika kileleni katika tendo ni pale amefika kiwango cha juu cha msisimko na raha katika tendo hilo. Mwanaume huanza kusisimka katika sehemu ya mbele ya dhakari na mwanamke huwa na sehemu maalumu.

Msisimko hubebwa na mishipa ya fahamu ya kiuno, uti wa mgongo hadi katika ubongo ambapo kiwango cha juu hufikiwa na mwanaume hutoa manii na mwanamke hutoa majimaji sehemu ya siri.

Mwanamke hufikia mwisho wa tendo kwa muda huo lakini kutokana na hali ya kimaumbile mwanamke anaweza kuendelea na akafikia tena na tena kileleni.Mwanamke ana sehemu maalumu ukeni ambazo zinapopata mguso na msuguano humwezesha afike kileleni. 


Sehemu hizi kitaalamu zinaitwa ‘Grafenberg Spot’ au G. spot. Sehemu hii inapatikana ukeni kwa ndani. Iligunduliwa miaka ya nyuma na daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama wa Ujerumani aitwaye Ernest Grafenberg.Sehemu hii inamletea mwanamke msisimko wa nguvu na kumfanya amalizie raha yake ya kujamiiana kwa kishindo kikubwa ‘ Powerful Orgasm’ na kutoa majimaji ukeni ‘Female ejaculation’.

Majimaji haya yanapomtoka mwanamke bado haijajulikana hasa yanatoka sehemu gani katika eneo hilo ingawa baadhi wanasema ni mkojo unatoka mara moja kwa kishindo, wengine wanasema yanatoka katika vitezi vidogo nyuma ya njia ya mkojo ‘Paraurethral ducts’ .Vitezi hivi pia baadhi ya wataalamu huvifananisha na tezi dume kwa mwanaume, kwani kazi ya tezi dume ni kutoa majimaji au manii wakati wa kufikia mshindo au kilele. Ili kuamsha G. spot mwanamke afike kileleni inatakkiwa uume uwe na nguvu za kutosha vinginevyo ni vigumu kufikia hapo.


CHANZO CHA TATIZO

Chanzo kikuu kinachoweza kumsababishia mwanamke asifike kileleni au achelewe kufika hapo ni sababu za kimazingira na kisaikolojia, ‘Situational and Psychological factors’. Vile vile zipo sababu za magonjwa au mifumo ya mwili mfano, mfumo wa fahamu na homoni.Kiasi kikubwa cha tatizo hili hutokana na matatizo yanayo-mzunguka mwanamke kama vile, maandalizi duni ya tendo la ndoa kwa kutozingatia kanuni na mwanamke kuingiliwa kabla ya kuwa tayari na hii inaweza kuwa ni kila mara. Kutokuamsha viungo vyake vya uzazi kwa ajili ya tendo

‘Insufficient foreplay’, tatizo jingine ni wote wawili mume na mke kutojua mapenzi na kazi ya viungo vyao vya uzazi, kutofahamu aina au njia mbalimbali za romance hivyo kusababisha mgongano mengine ni kutoelewa au kupenda kama mwenzake anavyohitaji, matatizo au migongano katika mahusiano, kujihisi vibaya pale unaposhindwa kumudu tendo la ndoa, kuogopa kuachwa au kukimbiwa unapohisi hufurahii tendo na huwezi kufika kileleni, kulichukia tendo lenyewe hasa endapo ulishawahi kupata matatizo nalo kama kubakwa au kuingiliwa kinyume na maumbile, na endapo kama una matatizo mazito ya kisaikolojia mfano ‘Depression’.


ATHARI ZA TATIZO
Mwanamke ambaye hafiki kileleni wakati wa tendo la ndoa, yupo hatarini kupoteza hamu ya tendo la ndoa hivyo basi kukosa msisimko wa tendo naieleweke kwamba, mwanamke ambaye hafiki kileleni hupata hamu kama kawaida pale tatizo linapoanza , pia hupata msisimko ambao haufiki mshindo kutokana na kukatizwa na mumewe endapo mumewe anawahi kumaliza tendo, au na hali ya mazingira na kisaikolojia. Hali hii inapoendelea mara kwa mara mwishowe mwanamke huyu hupoteza kabisa uwezo wa kumaliza tendo kwa mshindo au kufikia kileleni yaani ‘climax’.


Tatizo linapoendelea husababisha mwanamke awe anapata maumivu wakati wa tendo la ndoa. Maumivu haya hutokana na woga au wasiwasi hivyo kusababisha uke uwe mkavu na misuli yake hubana hivyo hata uume unashindwa kupenya.


MATIBABU
Hufanyika baada ya uchunguzi wa kina katikaa hospitali ambapo vipimo mbalimbali vitafanyika. Daktari atakuelekeza njia mbalimbali za mguso wa kuamsha hisia na msisimko ili kukuwezesha kufikia kileleni na kurudisha furaha yako na kama hujawahi kuipata basi utaipata. Njia hizi ni njia ya kujiamsha mwenyewe hisia ‘ Self – stimulation,’ njia nyingine ni kama vile ‘Relaxation techniques’ na ‘Sensate focus exercises’.


Njia nyingine ni kupata elimu na upeo kuhusu mapenzi, tiba nyingine ni za kisaikolojia kutambua na jinsi ya kuepuka migongano katika mahusiano ya kimapenzi.

Njia rahisi za kuwavutia wanawake kihisia na kufanya wakupende, Je unazijua?

“Saa nyingine ni vitu vidogo vidogo tu ndo vinavyotengeneza mshiko mkubwa kihisia, sifa moja ya akili au ishara ndogo tu inaweza kumshika kihisia mwanamke, vile vile ukitoa sifa mbaya ndo mwisho wako!.”Mwanamke hutumia muda mdogo sana kuamua kama una uzito wowote wa kumfanya yeye atoke na wewe kutokana na vitu vidogo vidogo unavyofanya na vile ambavyo huvifanyi ndo vinamsaidia kufikia kwenye maamuzi yake.


kiumeni.com imejaribu kukusanya njia rahisi za kumshika kihisia mwanamke ambazo sio ngumu wala za kupoteza mda na zitatoa tofauti kubwa kati ya kuangaliwa vibaya na kupewa namba ya simu…

  • Msifie kwa kitu kizuri…

Ukimwambia mwanamke anaharufu nzuri inayosambaza furaha, kutamfanya ajisikie vizuri, harufu ya furaha ni harufu ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo kila saa, hii itakufanya upate wasaa wa kumuuliza vitu gani kwenye maisha yake vinavyomfanya awe na furaha?, ambapo swali hili litamfanya avutiwe zaidi na maongezi yako na kujisikia vizuri zaidi, ukimsifia kwa kitu kizuri unakua mwanzo mzuri utakaokupa fursa na nafasi nzuri zaidi ya kuendelea nae kimaongezi.

  • Muombe ushauri…

Wanawake wanapenda sana kutoa ushauri na wanavutika zaidi kwenye njia hii maana utamfanye apate hisia umeona kitu kizuri kwake mpaka ukampatia hio heshima ya kumuomba ushauri, kuwa mwangalifu hapa maana hautakiwi kuonekana kama haujui kabisa juu ya kitu unachomuomba ushauri na hakikisha usifanye asijisikie vizuri. 
Ukiwa unaomba ushauri onyesha na wewe ulikua unafikiriaje juu ya hicho kitu au jambo ulilokua unaombea ushauri, na maswali yawe ya urahisi ambayo atatoa majibu kwa urahisi zaidi na hatimaye kuanzisha mazungumzo mengine.

  • Msifie kwa jinsi anavyoonekana…

Unatakiwa wakati ukitoa sifa, sifa ionekane ni ya ukarimu na sio vinginevyo, kwa hio inabidi utoe sifa ambayo ni ya asilia, kwa mfano usitoe sifa kama “Unamacho mazuri sana!”, jaribu kusema “umependeza kwenye hio nguo uliyoivaa!”. Ni njia nzuri ya kumwambia kuwa ni mrembo kuliko njia ya kwanza ambayo inaonyesha wazi sehemu mazungumzo yako yanakoelekea.

  • Mfungulie mlango…

Kumfungulia mrango mwanamke ni kitendo cha kiungwana sana, jionyeshe uungwana wako.

  • Muulize maswali…

Ukiwa unataka kumjua msichana ni lazima ufanye unachoweza ili kumfanya ajisikie vizuri, hii inamaanisha kuelekeza maongezi kwenye mambo ambayo ukiiyaongelea atajisikia vizuri na kwenye mazingira aliyoyazoea, unaweza kuelekeza maongezi yamuhusu yeye mwenyewe, wanawake wanapenda sana kujiongelea kuhusu wao wenyewe.
Ukimuuliza maswali juu ya maisha yake ya zamani na vitu anavyovipendelea utamfanya aongee kwa kujiamini zaidi, huku ukionyesha hamasa zako zipo sio tu kwa ajiri ya muonekano wake.

  • Puuzia simu yako…

Hakuna kitu kibaya kinachoonyesha mtu ulienae hana umuhimu kama kupokea simu au kusoma meseji katikati ya maongezi, ukiwa unaongea na msichana fanya akuone kama kuna mtu anakupigia na uikate simu mbele yake na kizima kabisa, akikuuliza kwanini umefanya kitendo hicho, mwambie mazungumzo yake yamekuvutia na unataka umsikilize yeye kwanza mengine  hayana umuhimu, utamfanya ajisikie na thamani kubwa sana kwako.

  • Ongea na marafiki zake na jihusishe kwenye mazungumzo yao…

Ukiwa unafikiria kumtongoza msichana, lazima utakua unatathimini utu wake, muonekano wake na mengineyo kama uwezo wake wa kuelewa mambo na kufurahi, ndivyo hivyo hivyo mwanamke nae anatathimini, na hututathimini ni kiasi gani ambacho tunaendana na jamii yake.
Wanawake huvutiwa na mwanaume mcheshi, anayependeka kwa urahisi na ni mtu wa kijamii, kwa hio jiingize kwenye maongezi na rafiki zake na ukiweza kuwavutia rafiki zake, utakua umemvutia na yeye pia, hakikisha kipindi chote cha maongezi, uwe umeweka wazi kwamba yeye ndio vutio lako kubwa.

  • Kuwa katika hali ya usafi na uvaaji mzuri na wakupendeza…

Wanawake wanapenda wanaume watanashati, wanapenda kuwaona wakiwa wanapendeza na kunukia vizuri mda wote na nywele zilizo katika hali nzuri.
Hembu fikiria wewe unawatathimini wao kwa muonekano, kwa nini na wao wasifanye hivyo vivyo?.

  • Mwangalie machoni…

Ni majaribu makubwa kutomwangalia mwanamke mzuri toka juu mpaka chini, anavyokua mzuri zaidi ndivyo ilivyo ngumu kuweka akili yako kwenye maongezi, hakikisha unamwangalia machoni, akikukamata unaangalia maziwa yake wakati anakupa stori kuhusu mama yake ujue atakuona kuwa wewe ni wa ajabu sana na moja kwa moja atajua umekuja kwake kwa ajiri ya kilichopo katikati ya miguu yake tu.

Vitu 12 ambavyo wanaume wengi sana huvifanya kitandani ambavyo huwafanya wanawake kuigiza wameridhika!.

Takwimu tofauti zinaonesha, na ni jambo ambalo hufaamika kwamba sio wanawake wote huwaga wanafika kileleni kila wakati wanapofanyamapenzi!

Lakini pia, wanaume wengi hupenda kuigiza na kujifanya kwamba wao ni wataalam sana wa mapenzi!

Na wanaume wa haina hii, hujisifia kwamba wao ni wazuri kiasi gani kitandani, na kwamba hakuna mwanamke yeyote ambaye alishalala nae ambaye hajamfikisha kileleni!.

Sasa, najua hii inakushangaza kidogo. Si ndiyo?

Kama kila mwanamke hugushi kuridhika kimapenzi, hawa wanaume siyo waongo?, au wanawake hawa ni wataalamu sana wa kufeki hayo mambo?!.

Kwa nini wanawake wengi huigiza katika hili?

Lakini mara nyingi haya siyo makosa yao!.

Mara nyingi siyo makosa yao na haya ni makosa ya wanaume – ukurupukaji wa wanaume!.
Mwanaume anaweza kuwa mbinafsi, na anachokijali ni yeye mwenyewe kuridhika na kusahau kuwa mwanamke naye anahaki ya kuridhika na kufurahia tendo na hivyo anashindwa ku focus na anaishia katikati.

Tunapokuja katika suala la mapenzi au kufanya mapenzi, wanawake huwa na safari ndefu sana ya kufika kileleni tofauti na wanaume.

Kwa hiyo kama kweli unataka kumridhisha mwanamke kitandani, usiogope na pia usiwe na wasiwasi kwamba hautamfikisha kileleni, wala usikamie kumfikisha kileleni. Unachotakiwa ni kujali tu wewe na yeye muwe na good time kitandani – wote mfurahie tendo. Elewa kwamba, hiyo idea itakufanya ufanye maajabu katika mapenzi ambayo haukuwahi kuyafanya hapo awali.

Na baada ya hapo, utaweza kumfikisha kila mwanamke unayekuwa naye kitandani kiurahisi kama vile mto unavyotiririka katika mkondo wake!.  

Mambo 12 wanaume hukosea kitandani na kuwafanye wanawake kuigiza kuwa wameridhika – kimapenzi!

Hizi ni sababu za kwanini wanawake huamua kuigiza wameridhika kitandani, badala ya kweli kuridhika. Wakati mwingine, kwa kweli siyo makosa ya mwanaume. Lakini mwishowe licha ya hayo yote, bado makosa yanaonekana ni yake – mwanaume!

#1 Haupo vizuri katika ForePlay. Mwanaume anaweza huchukua sekunde chache kumvua mwanamke nguo zake za ndani. Lakini mwanamke ni kama chungu cha kupikia, huchukua muda kushika moto, lakini baada ya kupata moto, hutumia muda tena kupoteza joto lake hatakama moto umezimika. Kama hautaweza kumchezea viungo vyake vya mwili vizuri na kwa ustadi, hataweza kufurahia tendo na hivyo hutaweza kumfikisha kileleni.

#2 Haujui anataka nini kitandani. Hili ni tatizo la wanaume wengi. Wengi hufikiri hujua kila kitu kinachouhusu mwili wa mwanamke, na kila kitu kinacho msisimue mwanamke kwa haraka. Lakini ukweli ni kwamba, kila mwanamke ana angle yake na kila mwanamke anamatarajio yake kitandani. Tumia muda kumsoma, angalia muitikio wake unapokuwa umamchezea sehemu zake za mwili, na jifunze ni wapi panamsisimue zaidi. Usiwe na kimbelembele kwamba wewe ni mzoefu na ya kuwa unajua kitu kinachoweza kumsisimua kwa haraka – utaharibu brother!.

#3 Poteza ufahamu. Unapokuwa kitandani na mwanamke – inabidi ufahamu wako wa kawaida uuache nje. Usipofanya hivyo, mwanamke wako kwasababu anajua unampenda sana, na yeye anakupenda sana, hatakama hajaridhika, atajaribu kuigiza kuwa karidhika ili akufanye wewe ujisikie vizuri au kidume * wakati kimoyomoyo anatamani mwanaume ambaye agekuwa ana mfikisha kileleni badala ya kuigiza vile*.

#4 Unajilaumu. Kwa baadhi ya wanaume, huwa wanaangalia na kuzingatia kama kumfikisha mwanamke kileleni kama ni ushindi mkubwa – ni kweli. Na hii inawafanya wao kila baada ya game kuwauliza wanawake zao – umeridhika baby? Akikataa – unajilaumu kwa kuwa mbovu kitandani, kwa picha hiyo – wakati unaofuata huyo mwanamke lazima aigize kuwa karidhika ili ufurahi na uache kujilaumu.

#5 Unamlalamikia. Ulishawahi kumlalamikia mwanamke wako au mke wako kwamba hashughuliki vizuri wakati mnapokua kitandani? Je ulishawahi kumfokea kwa hasira na kumwambia maneno kama *kwanini haushughuliki? na kwanini husemi kama nakuridhisha kitandani?*!!!”. Hapo next time lazima awe feki babu!.

#6 Unakasirishwa mapema. Unaweza usimwambie kwamba umekasirika, lakini sura yako tu itamwambia kwamba haukufurahia kwa sababu yeye hajafika kileleni. Na kila wakati unavoonekana umekasirika, unamfanya naye ajisikie vibaya, kitu ambacho kitamfanye aigize kuwa anajisikia vizuri wakati hata chembe mawazo yake hayapo huko kabisa.

#7 Kuropoka. Kuna wakati unajikuta umeropoka neno ambalo halifai na hivyo linamfanya ashtuke na kupoteza mood kabisa wakati mpo katikati ya mapenzi. Na kwa maana hiyo, anajiona kama si kitu, au kituko na kukasirishwa nacho!

#8 Unamfanya ajisikie/ ajione yeye mbaya. Hili ni jambo ambalo wanawake wengi hawapendi kulijua/ kulitambua. Siku zote. Na ni ukweli ambaohautakiwi umwambie. Je unamfanya ajisikie yeye ni mbaya, aidha kwa kumtukana au kumuambia jinsi yeye alivyo mnene, au kumuangalia usoni kwa lisura libaya – ya kukasirishwa wakati amevua nguo zote? Kama utamfanya mwanamke ajione mbaya, kuna uwezekano mkubwa kuwa hatajisikia vizuri hivyo mawazo yake yote hayatakuwa katika mapenzi , yatakuwa yanawaza ulimchukuliaje ulivyomvua nguo. Hivyo kila kitu ata fake maana ulishamtoa kwenye mood!.

#9 Bwana mkubwa ni MKUBWA HASWA(Mashine). Ndiyo, kuna wakati unakua unajisifu kuwa mashine yako ni kubwa sana hivyo unajua kila mwanamke utamridhisha. Lakini bahati mbaya unakuta mwanamke wako – baby wake ni mdogo, hivyo inampa wakati mgumu wakati bwana MKUBWA anapenyeza pale, hivyo kwa sababu anasikia maumivu , atakua anajifanya anajisikia vizuri wakati wa kulia huku anaugulia maumivu. Ukijua wewe uko hivyo usifanye fujo bwana boss – kuwa mpole na mwendeshe taratibu.

#10 Unachelewa kumaliza mechi – Na hivyo anajaribu kukuharakisha umalize. Kama mwanamke wako anaona unahangaika, au unatoka jasho, au unajitahidi sana usije kkufika kileleni kabla yake, na yeye akiwa anajua hatafika kileleni mapema, lazima aigize ili akufanye wewe ujione mwanaume ya kwamba umemaliza mechi salama na mmemaliza wote.

#11 Ana aibika. Hili ni jambo ambalo lazima likukumbe katika mahusiano mapya. Kama mwanamke unaye date naye anajua kwamba inamchukuaga muda mrefu kufika kileleni , ili wewe usimuone kuwa ni mzigo huwa anaigiza ili usijisikie vibaya au usimuoe ana mapungufu – hivyo anataka umuone yeye ni kama wasichana wengine ambao wanafika kileleni!.

#12 Unatumia Pressure kubwa sana. Kama ulishawahi kujitapa kwake kwamba wewe ni fundi. Na yeye akajijenga kifikra kwamba mkilala wote lazima ataridhika na utamfikisha kileleni haraka iwezekanavyo. Mnapokuwa katika shighuli, inatokea tofauti japo anajitahidi kuwaza kuwa anafika kileleni – lakini bado mabo yanakuwa magumu, hapo atachoka na kuigiza kuwa kafika kileleni kwa sababu umeshamkatisha tamaa ya alichokuwa akifikiria mwanzo.

WANAWAKE WENYE HIPSI NA SHIDA WANAZOKABILIANA NAZO HIZI HAPA

Wanawake wengi wenye hips , ni wanawake ambao si kwa mwanaume tu hata kwa wanawake wenzie husifia kuwa fulani kajaliwa, ki maumbile, ni kweli wana mvuto wa pekee, humwagiwa sifa nyingi za urembo, lakini pia kwa upande mwingine wa shillingi ni matatizo tupu.Sifa:

1. Huwatesa sana wakina baba wanapokuwa katika vyombo vya usafiri kama daladala, treni, meli na ngalawa, mababa wengi hujawa na hisia kali za mahaba kiasi kwamba hupata mfadhaiko.

2. Hawana haraka sana kwani mwendo wao, hutembea kwa maringo, hata daladala likisimamia mbali hawawezi kukimbia kuwahi.

3. Hutongozwa wanaume watano kwa siku, hata wanaume wasiposema kitu angalau ukonyeza.

4. Ni wasikivu sana wakati wa kudate maana wengi ni warefu hupenda sana kukuinamia kusikia zaidi uliongealo.
Matatizo.

1. Kwa kuwa huwa wanavutia sana ni rahisi kurubuniwa kwani mwanamke yeye duniani hawezi kutongozwa watu elfu 2000 asimpende mmojawapo.

2. Hawana raha kwani ukodolewa sana macho na watu, si wanawake wala wanaume.

3. Upata magonjwa sana asa fungus kwani sehemu zao za siri hazipati hewa ya kutosha kufatana na kubanana kwa nyama na msuguano kila watembeapo.


4. Wana gharama sana kuwatunza kwa sababu hawatakiwi kutembea kwa muda mrefu kuogopa msuguana hivyo umuoapo ni lazima ughalimike usafiri au unatakiwa kumunulia skin taiti kila mara kwa kuwa zinahariibika muda mfupi sehemu ya mapaja.


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Mambo 15 ya kumfanyia mwanaume unaempenda akuwaze muda wote!

Kuweza kumpata na kumteka mwanaume akili zake siyo kazi rahisi.  Kwa masumbuko ya sasa kimaisha na ulimwengu ulivyoendelea kiteknologia kumfanya mwanaume unayempenda akupende sana inakuwa viumu kidogo! Huwezi kujua wanatafuta nini na ni nini wanakipenda hasa.

Mwanaume ni kiumbe cha ajabu na ni rahisi sana kumchota akili zake kama unampenda, japo wana 
mambo mengi sana magumu kuyagundua, lakini vitu wanavyovipenda kwa mwanamke vinafanana kwa karibia wote dunia nzima. Usinielewe vibaya, hapa siongelei muonekano wa nje/mwili, kwa sababu hiyo hutofautiana kati ya mwanaume na mwanaume. Nazungumzia mambo ambayo yatamfanya aachane na ramsha ramsha zake zingine zote abaki akikuangalia na kukutafakari na aseme “Daah kweli huyu ni mwanamke wa tofauti”

Unawezaje  kumfanya akupende na akuwaze muda wote?

Hatujasema kila kitu hapa kitafanikiwa kwa kila mwanaume, kwa sababu kama nilivyosema hapo awali, kila mwanaume ana utofauti wake. Lakini kwa haya mambo hautamfanya tu akupende lakini utamfanya awe anakuwaza muda wote.

#1 Kuwa original. Ndio ni kweli, usipitishe tu macho yako haraka haraka kusoma hii sentensi kwa sababu ni sentensi uliyoizoea kuisikia mara nyingi. Lakini ulishawahi kujiuliza kwanini ni kitu ambacho maranyingi hupendekezwa wakati unaanza uhusiano mpya?

Kwa sababu ni kweli! Ukiwa original ni kitu kikubwa sana kinachoweza kumfanya mwanaume wako akupende zaidi. Inatakiwa umuoneshe haswa wewe ni nani kutoka kwenye kiini cha ndani ya tabia yako, ukijifanya muigizaji baadae utaumbuka! Kuwa original kutamfanya mwanaume unayempenda akupende wewe kwa jinsi ulivyo.

Usijaribu kufanya maigizo fulani eti ukizani atakupenda zaidi kwa kuigiza huko. Ukweli ni kwamba atakuambia unazingua, wanaume wapo simple sana, lakini siyo wajinga kiasi cha kuwaigizia.

#2 Jiamini. Najua hii umeshazoea kuisikia pia. Kujiamini kunavutia. Inamaanisha unajitambua wewe ni nani na unataka dunia nzima ijue wewe ni nani – na wanaume hupenda hili. Achana na madhaifu yako yote na jiamini ulivyo lazima atakupenda tu.

#3 Jiheshimu. Hakuna kitu kisichovutia kwa wanaume kama mwanamke asiye jiheshimu. Wanaume hujua- kama unaweza ukaonesha tabia za kutokujiheshimu mwenyewe – unawezaje kumshawishi kwamba unaweza kuwaheshimu wengine? Kwa wewe kujiheshimu kutamfanya macho yake na mawazo yake yakuwaze wewe tu!.

#4 Weka sheria zako na Viwango vyako wazi(Make your standard known). Kama umetoka na mwanaume na anataka arudi akalale na wewe siku hiyo hiyo, au siku ya pili au ya tatu na haujazoea kufanya hiv5o- mfanye atambue wewe siyo wa hivyo!. Kama kweli unataka asihangaike na wengine na kwenda kutembea na wanawake wengine wakti bado mpo katika hatua ya “dating” mfanye ajue wewe sio wa kirahisi hivyo. Kwa kumueleza sheria zako, atavutiwa si tu kwa vile unajiheshimu, lakini ni kwavile unataka awe kwenye mstari akiwa na wewe.

#5 Kuwa Mpole, Mtulivu, Mwema. Unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza – anachokiona ndivyo atakavyokutafsiri. Kuwa mkarimu na mpole ni kitu kikubwa sana mwanaume atakachovutiwa nacho kwako. Kama wewe ni mkarimu kwake na kwa watu wanaomzunguka, ata assume kwamba wewe ni mkarim kwa ujumla, na wanaume sikuzote hutafuta lulu ya hivi kwa mwanamke.

#6 Kuwa muelekezi. Hii haimaanishi uwe bosi! Usifanye hayo makosa. Wakati baadhi ya wanaume wanaweza kuipenda hiyo tabia(wachache sana), ila hubadilisha mambo baada ya mjda fulani. Kuwa unatoa amri ni moja wapo ya njia zitakazomuonesha unaweza kuwa kiongozi / msimamizi wa kitu fulani. Maranyingi , wanaume wengu hudhani kuwa wao ndoyo mara nyingi wanatakiwa kuwa viongozi kwa kila jambo, na ni kweli huwa ni vizuri anapoagiza jambo na mwanamke analitekeleza lakini na wewe uoneshe unaweza kusimamia unachoelekezwa nae!

#7 Jijali wewe na mambo yako. Simaanishi uwe unaishi kama miss Africa – Hapana! Ninachosema unatakiwa uyaweke mambo yako katika muundo na mpangilio unaoeleweka ambao ni rafiki kwako na mambo yako. Fanya mazoezi, kula vizuri, na kuwa msafi ni tabia ambazo wanaume wengi huvutiwa nazo. Kwanini? Kwa sababu inamaanisha hautaki tu ufanye kazi zako lakini ufanye uku hali yako ya afya ikiwa inaimarika, lakini pia uwe wa kupendeza na kunukia vizuri karibu yake.
Kama ataona unajijali, atajua ua uwezo mkubwa wa kujiwajibisha – kitu ambacho hukipenda sana.
#8 Usiwe wa kusomeka haraka. Usijaribu saana kumfanya yeye akupende. Kuwa makini sana na matendo yako wakati upo mbele yake – asikusome lengo lako hasa ni nini. Mfanye awe na maswali juu yako ya kuwa wewe ni wa aina gani. Hii itampa picha ya kwamba unajijali wewe na mambo yako lakini pia unatambua uwepo wake.

#9 Kuwa muwazi. Ni ngumu sana kwa mwanaume kukupenda na kumteka mawazo yake kama hakujui vizuri!. Funguka kwake. Sasa usianze kuropoka mambo yote yanayokuhusu kwake – utaharibu. Hatajali eti kwamba wewe kuna jamaa alikukatili wiki moja iliyopita na akakufanya ulie siku nzima.

Mwambie matazamio yako, malengo yako na ndoto zako. Mpe mawazo na mitazamo yako kwa baadhi ya mambo yanayoendelea katika jamii inayowazunguka au hata katika nchi. Kwa kumfanya akujue wewe ni wa aina gani , na ndoto zako na malengo yako, itamfanya akuone wewe wa tofauti na shujaa! Niamini.

#10 Usitabirike. Kwa suprise unaweza kwenda nyumbani kwake na pizza, au wyne, au bia, au keki. Siyo tu atavikubali, lakini utamfanya awe kichaa zaidi juu yako. Kuwa unatabirika mara nyingi kuna udhi, na atakuchoka mapema. Kwa kuendelea kum-suprise kutamfanya awe hana ujanja kwako na atakuwa anatamani ajue utafanya nini wakati ujao!]

#11 Kuwa Bize! Kuwa na maisha yako! Kwa mshangao, wanaume hujikuta wakiwapenda wanawake ambao huwa bize na mambo yao. Inamaanisha hauhitaji mtu mwingine yeyote kutoka pembeni aje akupangie au akusaidie maisha yako – unajitosheleza mwenyewe. Kuwa unafanya mambo yako na kufata hobby zako kutamfanya yeye ajaribu kutafuta muda ambao upo free ili akujue zaidi mana umemvutia.

#12 Usiwe mtu wa kujitengeneza sana. Wanaume huwachukia sana mwanamke ambaye anatumia saa nzima kufanya makeup. Hii hajahesabia bado muda wa kuoga, kutengeneza nywele, kuchagua nguo ya kuvaa na kuvaa kwenyewe. Simaanishi usifanye haya mambo, lakini mwnaume humchukia mwanamke ambaye muda wote lazima apigiwe kelele ili afanye jambo fulani au lazima aitwe ili awe haraka. Kama unajua wewe ni wa hivyo jitahidi sana asikusome – na ikitokea iwe mara moja moja sana tena kwa sababu maalum.

#13 Mkubali. Kama kweli unataka kumdatisha basi mkubali yeye alivyo. Wakati mwanaume anajisikia kuwa anaweza kuwa yeye ‘original’ akiwa na wewe bila wasiwasi wowote wala kuficha chochote, atajisikia kama kashushwa kwenye dimbwi la mapenzi..hahah!.

#14 Jitahidi kumsapoti kwa mambo yake anayofanya. Hatakama kazi ni ngumu kiasi gani wewe jitahidi hata kidogo kumuonesha kuwa unamuunga mkono kwa jambo analolifanya kwa sababu unajua ni la manufaa kwa wote. Hii itamtia moyo na atatamani awe na wewe muda wote.

#15 Endelea kuzifuata ndoto zako. Kama ulitaka kwenda Ulaya, au kuandika kitabu, au kuwa mfanyakazi bora ofisini kwenu, usiache, endelea kufight hatakama jamaa yako yupo kijijini analima, wewe nawe endelea kupambana. Hapa inaweza onekana unapingana nae lakini kama nimuelewa atajua wewe ni dhahabu unayopaswa kuchungwa kwa jicho la pekee. Na nani anajua kwani? Labda na yeye kwa siri amepanga akaishi ulaya. Kwa yeye kujua ambitions ‘matarajio’ yako kutampa hamasa ya kufanya kazi zaidi ili wote mwishoni mfurahi.

Wanaume wanaweza kuwa watu wagumu kuwasoma, na kuwashawishi yataka moyo. Japokuwa kila mwanaume atapata kitu tofauti anachokipenda kwa mwanamke, lakini haya mambo 15 yamethibitika kumdatisha mwanaume yeyote yule hatakama ana moyo wa jiwe- Kwa Tricks hizo moyo wake hautasukuma damu peke yake – Utakuwa na jukumu la kukusukuma na wewe pia!.

Kama imekufungua na imekusaidia kujibu maswali mengi uliyokuwa ukijiuliza basi share na mwenzako ili imsaidie kama ilivyokusaidia wewe.

Jinsi Ya Kumdhaifisha Mwanamke Ili Akupende

Ikija katika maswala ya udhaifu katika mwanamke, huwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwa tofauti katika kila mwanamke.

Hebu mwanzo tuanze kwa kusema kuwa kila mwanamke yuko tofauti. Si kila mwanamke anataka kitu kimoja kwa kila mwanaume. Lakini, kuna baadhi ya mambo ambayo huwa yanajitokeza juu zaidi katika udhaifu wa mwanamke. Kama mwanaume atafanya mambo vile ambavyo inahitajika, basi itakuwa vigumu kwa mwanamke kuukwepa mtego.

Mambo ambayo haswa huwafanya wanawake kuvutiwa na wanaume huwa ni tabia flani ambazo hujitokeza. Hii ni kumaanisha kuwa kila mwanamke huwa amemakinika zaidi kwa mambo ambayo mwanaume hufanya tofauti na sura yake.

Wakati unapotongoza mwanamke lazima ujenge connection ya kihisia zaidi. Hii ni kwa sababu kujenga muungano wa kihisia na mwanamke hudumu zaidi ukilinganisha na umbo lako. Kile kitu ambacho unahitaji zaidi katika mahusiano yako ni kuwa na muungano wa kihisia.

Kama kweli unataka kumvutia mwanamke, unahitaji kuwa mdhaifu wake. Kama atashindwa kujizuia na kuvutiwa kwako, basi utakuwa na nafasi rahisi ya kuuteka moyo wake. Lakini kwanza, unapaswa kujua ni nini haswa kinachochangia hadi mwanamke kuwa mdhaifu mbele yao. Haya hapa ni mambo ambayo humfanya mwanamke kuwa mdhaifu.
#1 Kuwa mkarimu wa ukweli. Hauwezi kufeki jambo hili. Wanawake kwa kawaida huvutiwa na wanaume ambao wanaonyesha ukarimu wa ukweli. Ukiwa mkarimu kwa wengine, itamuonyesha mwanamke vile ambavyo utamchukulia. Huu ni udhaifu mkuu kwa kila mwanamke.

#2 Tabia za usaidizi. Udhaifu wa kila mwanamke ni kuwa na mwanaume msaidivu. Wakiwa wanapewa sapoti na mtu, huwa kawaida wanavutiwa na mtu kama huyo. Kuna kitu ambacho hujitokeza ndani yako wakati kuna mtu anajitokeza na kukusaidia katika maisha yako. Kwa mwanamke huwa maradufu. Usaidivu wako kwa mwanamke kunamfanya awe dhaifu kwako.

#3 Kushangilia mambo anayotimiza katika maisha yake. Kwa kuongezea usaidivu wako, wanawake hupenda mtu ambaye anafurahia na kushangilia mambo ambayo anatimiza maishani mwake. Wakati wamepandishwa cheo kazini ama amemaliza kufanya mradi wake, kukiwa na mtu karibu yake ambaye atashangilia mafanikio yake kila wakati ni jambo ambalo kila mwanamke anatamani.

#4  Kupendezwa na hamu zake. Hii haimaanishi kuwa udhaifu wa kila mwanamke ni kuiga kila kitu ambacho anapenda, la. Hii ni ile hatua ambayo unakuwa na interest na mambo muhimu ambayo huyapenda zaidi katika maisha yake. Kwa mfano ukimwona mwanamke anapenda sana mchezo wa magongo ama anapenda kufuatilia maisha wa wasanii aina flani, basi wewe jifunze kucheza mchezo wa magongo na pia uanze kuwatambua wasanii husika. Akiona kuwa unapenda mambo ambayo anapenda utakuwa umemdhaifisha.

Haya ndio mambo muhimu ya kuzingatia kama unataka kumfanya mwanamke adhaifike mbele yako. Kando na mambo hayo manne makuu unapaswa kujihami na mambo haya ambayo yatakufanya uuteke moyo wake:

#1 Lazima uwe mmakinivu na maswala yake ya ndani. Wakati mwingine wanaume huchoshwa kusikia malalamishi ya mwanamke lakini siri kuu ya kumteka mwanamke ni kuwa msikivu kwa kila kitu anachokuambia coz atakuona kama jangina wake wa maisha.

#2 Mpe saport kwa kila kitu. Kuna wakati anaweza kuongea mambo ambayo kwa msingi unaona kuwa hawezi kutimiza. Akifikia hapo wewe unapaswa kunyamaza tu. Unapaswa umpe sapoti kwa kila kitu. Haijalishi kama unamuelewa au la, unapaswa umsaidie tu.  Bora tu mambo yake anayojaribu kutimiza hayamdhuru yeyote ama yeye mwenyewe.

#3 Muulize maswali. Unaweza kuona labda jambo hili halina maana yeyote. Lakini ukiwa unamuuliza maswali mara kwa mara kuhusiana na miradi yake ama mambo anayofanya siku baada ya nyingine utakuja kumuelewa zaidi. Hii itasaidia kwa sababu atakuona unajihusisha na maswala yale ya maisha hivyo atavutiwa na wewe na utatumia swala hili kama udhaifu wake.

Upo!?

Fahamu kuhusu tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa

Ndugu zangu leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Tutajadili sababu zinasababisha mwanaume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa au kuongeza hamu.

Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa. Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka.

Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi, SIYO LAZIMA kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.

Ukubwa wa tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
Wanaume wengi hawapendi kulizungumzia tatizo hili waziwazi na hata wanawake pia. Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, kwa lugha nyepesi kuna mwanamme mmoja mwenye tatizo hili baina ya kila wanaume sita au saba.

Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hunyongea wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake. Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi limebainika kuwa ndilo linaloongoza katika kuleta migogoro ya unyumba kuliko matatizo mengine yote.

Utajuaje Kama Una Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa?
Tatizo hili halitokei ghafla kama vile umelala halafu ghafla asubuhi unaamka una mafua, la hasha. Ni kitu kinachotekea pole pole na pengine mwenyewe usijigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita au miezi kadhaa iliyopita.

Vile vile kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani haimaanishi kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, pengine una hamu thabiti lakini mazingira hayakukuruhusu. Lakini iwapo hakuna kikwazo cho chote na upo na mwenzi wako halafu inapita wiki bila kufanya tendo la ndoa au unalifanya tendo hilo mara moja au mbili tu kwa mwezi, inabidi uanze kujiuliza maswali.

Lakini ieleweke pia kuwa kuhesabu umefanya tendo la ndoa mara ngapi katika kipindi fulani si kipimo pekee cha tatizo hili. Mawazo yako kwa ujumla kuhusu tendo hili ni muhimu pia – jinsi unavyolichukulia na kuliwazia tendo hili kabla, wakati wa tendo na baada ya kumaliza tendo ni muhimu katika kujipima.

Viashiria vingine vyaweza kuwa: kumtomasa mkeo mkiwa ndani tu – chumbani na si penginepo. Iwapo tendo hili unalifanya pale tu mwezi wako anapokuanza na huwa unalifanya kama mazoea bila kuwa na mawazo ya kushiriki kikamilifu.

Kama humwazii mpenzi wako anapokuwa hayupo kwamba angekuwapo ungeweza kufanya naye tendo la ndoa. Vitu hivi kama vinakutokea basi kuna dalili za kuwa unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na kwamba inabidi utafute suluhisho.

Sababu za mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.

Mahusiano baina ya mwanamme na mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako? Huna wasiwasiwo wote na mahusiano yenu? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.

Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.

Kama kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua. Kwa mfano, kama mwanamme unawahi kufika kileleni au una matatizo ya jongoo wako kupanda mtungi, tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya. Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.

Mawazo mengi na uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. Kama unabenwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.

Msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.

Matumizi ya madawa na pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Umri kuwa mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanammme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo katika mfumo wa homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.

Matatizo ya kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa uwezo wa kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake baada ya kuona kile anachokitaka hakipati kwa mpenzi wake.

Yafuatayo ni mambo matano ambayo wanawake wanapenda waume zao wayafanye:

1. Wanawake wanapenda ufuate wanayoyataka
Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu. Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanya vile wanavyovipenda.

2. Hupendelea tendo la ndoa lidumu muda mrefu
Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda kuungana na wewe kihisia kupitia kushikana, kubusu nakadhalika. Wakati wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka. Kwa hiyo wanapenda tendo la ndoa lidumu lakini lisichoshe.

3. Wanataka mwanaume jasiri sio anayetumia nguvu
Wanawake wanataka wanaume walio jasiri wa kufanya nasio wanaotumia nguvu na ubabe. Wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu na mwisho kuwaumiza wapenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. Wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri kwamba sio kutumia nguvu na ubabe.

4. Wanawake hawafanani
Wanawake wanapenda wanaume wajue kuwa sio wanawake wote hupenda vitu sawa. Wanaume wengine hufikiri kuwa kwa sababu mpenzi wake wa zamani alikua anapenda kufanyiwa alikuwa basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta njia ya kukukwepa. Kwa hiyo mwanamme anatakiwa amjue mpenzi wake kibinafsi yeye kama yeye na sio kumjua kwa kumfananisha na wanawake wengine. Mwanamme amfanyie mpenzi wake kama anavyopendelea na sio kama anavyofikiri wanawake wanapendelea.

5. Kumfurahisha mwanamke sio ufundi tu bali ni mapenzi ya dhati
Wanawake wanapenda kuonyeshwa upendo au mapenzi ya dhati. Wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi na uzoefu katika haya mapenzi, ila wanasema hiyo sio kitu bora zaidi, wanachokitaka ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Mapenzi ni kichocheo kikubwa cha kumridhisha mwanamke.

YAJUE MAMBO MANNE YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia

. Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi.

Nawakaribisha sana!

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia. 

Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa.

Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.

Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.

Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha? 
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.

Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako. 
Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.

Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.

Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika.

Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.

Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu. Niwatakie siku njema na tukutane wiki ijayo!

Design a site like this with WordPress.com
Get started