Kuwa na wapenzi wengi ni tatizo la kisaikolojia

Katika ulimwengu wa sasa kuwa na uhusiano wa mapenzi na zaidi ya mtu mmoja ni kitu cha kawaida sana. Hapa nikilenga jinsia zote kuanzia wale walio ndani ya ndoa na ambao bado.

ILIVYOZOELEKA

Awali wanaume ambao kiasili huongozwa na tamaa ya muda mfupi ya kufanya mapenzi ndiyo pekee waliokuwa wakihusishwa na wapenzi wengi suala ambalo hata kisayansi linathibitishwa hivyo kutokana na utofauti wa maumbile kati yao na wanawake.

WANAWAKE WAMEINGIA

Lakini siku hizi hata wanawake nao hawapo nyuma. Wengi wao wamekuwa wakijiingiza kwenye uhusiano wa wapenzi zaidi ya mmoja kutokana na madai ya kuumizwa na wanaume wao ambao wamekuwa wakiwasaliti kila kukicha kiasi cha kushindwa kuwatimizia mahitaji kadhaa hasa suala la unyumba.

WASIOOLEWA PIA

Hata hivyo, tafiti zimeonesha kwamba, asilimia 78 ya wasichana wa kuanzia miaka 17 hadi 25 ambao hawajaolewa nao wamekuwa na kasumba ya kutotulia na mpenzi mmoja kwa kuwa huhitaji wanaume wenye uwezo kifedha ambao huwatimizia mahitaji yao na wakati huohuo wakitaka kuwa na wale wanaowapenda kwa dhati.

MADHARA YAKE SASA

Kusheheni wapenzi kuna madhara mengi ambayo yanafahamika, kama vile kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na Ukimwi, lakini kitu ambacho wengi hawakifahamu ni kwamba, kumiliki wapenzi wengi husababisha matatizo ya kisaikolojia. Hii ni kutokana na wahusika kukiuka hitaji la moyo la kuwa na mpenzi mmoja ambaye atamuamini na kuwa na lengo naye moja.

TWENDE NA TAFITI

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ikiwemo ile ya wanazuoni kutoka Chuo cha Dunedin nchini New Zealand ya mwaka 2007, ilionesha kuna matatizo ya kisaikolojia yanayotokana na mtu kuwa na wapenzi wengi kama ifuatavyo:Kushindwa kutosheka kihisia.

Wengi kati ya watu wanaojihusisha na wapenzi wengi waligundulika kuwa na tatizo hili ambapo kawaida hata walipokuwa tayari wameshakutanishwa na wapenzi wao faragha bado walionekana kutamani kuwa na wapenzi wapya pale wanapokutanishwa na watu wapya iwe wanaovutia zaidi kuliko wapenzi wao au lah!Tatizo jingine la kisaikolojia la wanaojihusisha na wapenzi wengi ni mwendelezo wa tatizo lililotajwa hapo juu ambapo mtu hujikuta akishindwa kutulia kabisa na mpenzi mmoja hata kama ataamua kufanya hivyo kutokana na majukumu.Kama hiyo haitoshi, tatizo kubwa zaidi linalowakuta watu hao huwa ni ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa wanapokuwa na wapenzi wao kwa muda mrefu kwa kuwa akili yao huzoea kuwa na wapenzi wapya ambao huwasisimua zaidi kuliko wa zamani ambao huwafanya wakinai polepole.

HITIMISHO

Kwa hiyo kama wewe unajijua huwezi kuwa na mpenzi mmoja mpaka uwe na mwingine na kuzidi kutafuta mwingine, ujue umeshaathirika kisaikolojia. Cha kufanya ni kujifunga kwa dhati huku moyo wako ukijua ni ugonjwa na tiba yake ni kuachana na wapenzi wengi, baada ya muda utazoea.

Unayetembea na Mume, Mke wa Mtu Hii Inakuhusu Sana !

LICHA ya kuwepo na msemo wa mke au mume wa mtu ni sumu bado watu wengi wameendelea kutenda tendo hilo.

Hawahofii madhara yake. Wanaona kama ni jambo la kawaida. Wanahalalisha jambo hilo utafikiri kufanya hivyo ndiyo jambo jema.Kutembea na mke au mume wa mtu ni tabia. Huanza taratibu na baadaye hukua.

Kama vile ilivyo kwa mlamba asali, kadiri anavyopata utamu ndivyo anavyozidi kulamba. Kila anayefanya kitendo hiki huwa na sababu zake.


Kuna ambao wanaingia kwa sababu ya mawazo. Alikuwa na mpenzi au mchumba wake wakaachana, ghafla anajikuta ameingia katika penzi la mke au mume wa mtu kwa sababu ndiye aliyempata kwa wakati huo.

Wengine wanaingia katika janga hili kwa sababu ya tamaa tu. Wengi sana wanaingia kwa sifa hii. Wanataka maisha mazuri hivyo wakiyaona yanapatikana kwa mke au mume wa mtu, wanaingi. Hawaangilii matokeo ya baadaye, zaidi tamaa ndizo zinazomuongoza.

Hapo ndipo unapokuta mwanamke anapokubali kufanywa chombo cha starehe. Mume wa mtu anayetembea naye anamtumia kama chombo cha kumuondoa mawazo yake. Anamfanya kama chombo cha kumstarehesha pale anapokuwa amegombana na mkewe.


Bahati mbaya zaidi mwanaume wa aina hiyo hupenda kuumiliki huo mchepuko wake. Hataki amuone na mwanaume mwingine. Anahakikisha kwa kila namna anamfunga kwa kila njia anayoijua ilimradi asichepuke.


Anahakikisha anampatia kila kitu. Kama ni fedha, nyumba na hata magari ya kifahari anampa. Anafanya hivyo ili asisalitiwe. Na akithubutu kufanya hivyo lazima mhusika akione cha moto. Hapo mwanamke hana ujanja, anakubali kuepusha shari.

Matokeo yake anajikuta anapoteza muda. Anashikiliwa na mtu ambaye tayari ana mtu wake rasmi. Yeye ni wa ziada lakini mwanaume anamfunga asipate mtu mwingine. Atazalishwa, atalea watoto na kujikuta uzee ukimnyemelea pasipo kuwa na ndoa.

Vivyo kwa wanaume, nao wanapoteza muda. Wanajikuta wameshikiliwa na wanawake wenye fedha.

Hawataki wawe na wanawake wengine. Wanaume hao nao pia hupoteza muda. Lakini wengine huingia kwenye tabia hii kwa tamaa za kimwili.
Kila anayekutana naye anataka awe wake.

Haijalishi ni mke au mume wa mtu, yeye anamtamani na kumtaka awe wake. Marafiki zangu, kuna kila sababu kila mmoja wetu kujiuliza mara mbilimbili kabla hujaamua kuchepuka na mume au mke wa mtu.
Fikiri kuhusu madhara ya kupoteza muda.

Fikiri kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye. Utatumika hadi lini? Utakuwa mtumwa wa fedha hadi lini? Tamaa zako zitakufikisha wapi? Kwa nini usimpate wako? Utakayekuwa na uhuru naye.

Mume au mke wa mtu huwezi kuwa na uhuru naye. Atatumia muda mchache kwako lakini bado atalazimika kuihudumia familia yake. Wewe utabaki kuwa wa ziada.

Bahati mbaya anakubana wewe usioe au kuolewa na mtu mwingine.


Kuna umuhimu wa wewe kuwa na mchumba wako. Mtakayeanza na kumaliza pamoja safari ya hapa duniani. Mtu ambaye mtaelewana kwa kila hali, mtafikia hatua ya kufunga ndoa na kulea familia yenu pamoja.
Utakuwa mtu wa wiziwizi.

Hujiamini. Utazaa au kuzalishwa watoto wa nje ya ndoa. Jambo hilo ni hatari pia katika mustakabali wa watoto. Ndoa wewe utazisikia kwa wenzako. Ni jukumu lako kuchagua njia iliyo sahihi. Kuchagua mwenza sahihi pasipo kusukumwa na jambo lolote.
Maisha ya uhusiano ni zaidi ya fedha. Uhusiano ni utu. Mtu ambaye mtajaliana kwa kila jambo. Katika shida na raha. Katika uzima na magonjwa, hayo ndiyo maisha mazuri ya uhusiano. Kinyume na hapo ni janga. Utafurahia maisha kwa kipindi fulani, baadaye utapata machungu.

Usiforce kupendwa ukiachwa achika

Waziwazi unaonyeshwa kuwa HUPENDWI,HUSIKILIZWI,UNAPIGWA,HUHITAJIKI,UNADHARAULIWA,UNASALITIWA,UNATUKANWA,UNAFUKUZWA,NA UNAKASHIFIWA,,,,, Umemaliza ndugu wote kwa kuwapa malalamiko ya matendo ya mwenza wako bado hajabadilika,,,,

mpaka imefikia hatua hata ndugu na marafiki hawapokei tena simu zako,,,,,kwa kujua wazi simu zako wewe ni za malalamiko tu,,,,,

lakini bado umeng’ang’ana kama ruba huku ukijiona mvumilivu,,,,,,,

huo sio UVUMILIVU huo ni UTUMWA#USIFORCEKUPENDWAUKIACHWAACHIKA.

Hii ndio Thamani ya MWANAMKE

Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu,
unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako.

Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo.

Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua,
kwenye baridi tunatamani pia jua, Hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele.

Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na
vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini
unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe
nenda tu tafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani ao watoto.

Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wameponaje, wanalia usiku hujui hata nani alikuwa
anawabembeleza, ukirudi unakuta nguo safi chumba kisafi hutoi hata shukurani kwakuwa ushasahau kua kuna mtu anasafisha siwe safi muda
wote.

Na anafanya vitu vyote hivyo kama Jua bila kelele lakini wewe ukitoa elfu mbili ya sukari utamnyanyasia mpaka ndugu zake kuwa unawalisha wewe! Hembu siku aondoke akuachie hao watoto unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako
na kumuambia hajaja na kitu, uanze kuwapikia na kuwaandaa kwenda shule, ufue nguo zao na zako.

Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini hawezi kufanya hata nusu ya kile anachokufanyia mkeo, kwani yeye
atafanya kama kazi lakini mkeo anafanya kwa mapenzi, hahitaji umlipe chochote zaidi ya kutimiza
majukumu yako na kumheshimu kama mke katika maisha yenu.

Vuta picha umeamka mkeo hayupo, watoto
wanataka kuogeshwa kunywa chai na kwenda shule, hapo unatakiwa kuwahi kazini na mchana watoto wale!

Mheshimu sana mkeo kuna mambo mengi ambayo anayafanya ukiambiwa uyafanye Wewe utachanganyikiwa na mkeo huyafanya kwa upendo. Mwanamke anachohitaji kwa mume ni upendo na heshima tu.

Mhudumie, mpe upendo, muheshimu na muonyeshe kuwa kwako ana umuhimu mkubwa, mfanye mkeo atabasamu kila mara na familia nzima
itatabasamu

Jinsi yakujua Mwanamke ambae hajatulia

Mwanamke ambaye ni muhuni kwa hapa mtaani kwetu huwa anaitwa majina mengi sana, wengine humuita danga, kicheche, kiwembe na mengineyo mengi.

Hata hivyo pamoja na kuwapo kwa majina hayo wengi wa wanaume bado hawajajua ni kwa namna gani wanaweza kumjua mwanamke ambaye hajatulia, makala haya ni jibu tosha.Hivi ndivyo utakavyoweza kumjua mwanamke ambaye hajatulia:

Siyo rahisi kupenda

Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye.

Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaishaWanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu fulani kutoka kwako.

Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote.

Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka. Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

Anamarafiki wakiume kwa manufaa

Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale.

Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka.Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka.

Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.

Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.

Share this:

Sirikubwa mpezi wako hatakiwi kuzijua

1. Idadi ya wapenzi wake wa zamani

Wanaume wengi hupenda kujua wao ni wangapi kuwa na mwanamke Fulani.

Lakini mwanamke kamwe hawezi akakwambia wewe ni wa ngapi. Kumuuliza jambo hili kunamkera sana mwanamke na ndio maana mara nyingi hawezi akakwambia ukweli.

2. Anakulinganisha na mpenzi wa zamani

Mwanamke mara nyingi anakulinganisha na mpenzi wake wa zamani japokuwa hawezi kukwambia waziwazi.

Wakati mwingine tabia hii huwafanya wanawake kuwatamani wapenzi wa zamani na hata kurudiana nao endapo watakosa mtu aliye bora kuliko mpenzi wake wa zamani.

3. Kasoro zako

Mwanamke kamwe hawezi kukwambia kasoro zako. Wanawake wanajua kumfichiaa mpenzi wao mambo wasiyotaka yajulikane kwa wengine na kwa mpenzi wake.

Wanajua njia za kiujanja za kutumia ili kufichua siri zako zote. Mwanamke hawezi kukwambia kasoro zako kwa kuogopa kukuumiza.

4. Mapungufu yake

Mwanamke hawezi kukwambia mapungufu yake labda kwa kuhofia kusheshwa thamani. Wanawake ni wasiri sana kwa mapungufu yao. Wanajua vyema hofu zinazomuandamana, vitu vinavyowakosesha usingizi na mambo yanayowalemea maishani japo sio rahisi kuonyesha. Kwa nje anaweza akaonekana yuko vizuri na hana tatizo kumbe ndani ana matatizo au mapungufu.

Anaweza kufanya yote kufunika upungufu wake!

5. Huwa unampagawisha mpaka anakosa la kusema

Hili halisemi kabisa mwanawake kwa sababu anaona haya kutumia maneno ya wazi kueleza raha unayompa. Maneno ya kuzuzua ni himaya ya wanaume, lakini wakati mwingine wapo wasioweza kuficha.

6. Haumridhishi katika tendo la ndoa

  1. Wanawake wengi hawapendi kusema kama hawaridhiki Kwenye tendo la ndoa. Wanawake wanahitaji kuandaliwa vilivyo kwa dakika 10, 20 ama nusu saa. Mara nyingine wanaume huwahi kabla mwanamke hajawa tayari na hivyo kushindwa kuridhika lakini hawezi kusema.

Zijue Hatua Za Kumfanya Mwanamke Akutamani

Ungehisi vipi kama kila unapoamka asubuhi mwanamke unayemjua anakuwa wa kwanza kukutumia jumbe za kimahaba na kukuambia, “Jana sikulala, nilikuwa nakufikiria wewe”?
Ama je, kila ukikutana na huyu mwanamke anakwambia, “bebi usiende, nataka muda mwingi na wewe. Nakumiss sana”?

Ni raha iliyoje hii?

Sasa fikiria ungekuwa na uwezo wa kufanyia hivi mwanamke yeyote yule unayekumbana naye! Ni nishati ya ajabu!

Uzuri hapa Nesi Mapenzi hatukosi kuja na ujanja mpya. Fuata mbinu hizi hakika 3 ambazo zitamfanya mwanamke yeyote akutamani.

#1 Kuwa wingu lisilofahamika.
Hii inamaana ya kuwa usikuwe na yeye wakati wote. Kama mmepanga kukutana na yeye ili muongee kwa saa limoja, hakikisha umekaa na yeye muda wa nusu saa halafu utoe kisababu cha kujiondoa katikati ya maongezi yenu. Hii itamfanya kuachwa kwenye mataa na kutaka kujiuliza maswali kama mungekuwa naye saa zima mngeongea nini. Hii itamfanya yeye kukufikiria kwa urahisi. Lile ambalo mmeliacha kati kati litakuwa likimzunguka akilini mwake.

#2 Uwe usukani.
Mwanamke yeyote, uwe uko na mahusiano naye au la, hakikisha kuwa wewe ndiye unayeamua mambo yote mtakayoyafanya mkiwa pamoja. Kama ni kuchagua sehemu ya kukaa, sehemu ya kula, sehemu ya kutoka ama chochote kile ambacho mnachotaka kufanya, wewe ndiye utakuwa ukiamua bila kumwachia nafasi yeyote ile. Huu ujanja utamfanya yeye kutofanya jambo lolote bila kukufikiria wewe. Yaani atakuwa hawezi kujiamulia mwenyewe hadi wewe uwe karibu yake. Hii moja kwa moja itakuwa njia rahisi ya kwake kukufikiria wakati wote ule atakapokuwa akifanya shughli zake.

#3 Kuwa mtu wa mwisho akilini mwake.
Utafiti umegundua ya kuwa kile kitu ambacho mtu hufikiria cha mwisho ndicho kitakachomjia ndotoni mwake. Na kama usiku wake umemuendea vizuri bila tatizo, basi asubuhi yake kitu hicho hicho kitakuwa bado kinamjia akilini. Mbinu hii inaweza kutumika vizuri kama utahakikisha ya kuwa wewe ndiye mtu wa mwisho kabisa ambaye anaongea naye…yaani unaweza kumpigia simu nyakati zake za kulala. Hii itamfanya yeye kuweza kukuota na kuchangia  kukufikiria siku ya pili. Hii ni njia nyingine rahisi ambayo itamfanya yeyote kukufikiria mara kwa mara.

Niamini, ukitumia mbinu hizi tatu vizuri, mwanamke yeyote atakuwa akikufikiria wewe mara kwa mara na inafanya kazi asilimia 100 bila shaka yeyote ile.

Ukiyaona haya Kwa mwenza wako tambua ana mtu nje

1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana)Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae! Anakutumia tu huyo !

2Sisi ni Marafiki tu!Kwa ambao bado hawajaoana Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.

Na kwa ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu!

3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu!Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi wako na ndio maana anakuwa hivyo!

Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani!

4.Mabadiliko ya Ratiba za KaziKwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na dharula za kikazi zisizoisha mara vikao mara n.k !

5. Kutumia Muda Mwingi katika ComputerKama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi za ofisini anamalizia!

6. Simu za Siri, Simu kuwa locked !Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa au inawekwa silent ! Pia mambo ya kulock simu na hizi SmartPhone sasa mtu akishatupia kitu cha Pattern/Password/PIN ndo basi tena unatakiwa kuwa mjanja sana kuweza kumkamata.!

7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka!Waswazi wanasema “Wasiwasi ndo Akili” Basi wasiwasi wako huenda ukakupa akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli!

Mambo 7 Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Hii Valentine’s Day

Siku ya Valentine ndio hio imetufikia. Wengi wamekuwa wakiongea kuhusiana na hii siku. Siku hii kwa wale ambao wanaisherehekea wanadai ni siku ya wapendanao. Wengi huichukulia siku hii ni spesho kwa wawili wapendanao kujumuika pamoja.

Well, kwa wale ambao wanaisherehekea siku hii, ni mambo gani ambayo unayafanya? Wengi watakuambia wanangojea jioni wakakutane na wapenzi wao waende dinner. Wengine wangesema wanawanunulia wapenzi wao maua, wengine wanasema watawasha mishumaa wakati wa jioni ili kuleta mazingira ya mahaba, na baadhi watadai watabikiri watu siku hio.

Hapa Nesi Mapenzi tuna wazo tofauti. Wazo letu ni kuwa unafaa kuspend siku nzima na mpenzi wako. Kama unahitajika kazini ama masomoni, siku hii itenge spesheli kwako na mpenzi wako, yaani kuanzia asubuhi hadi usiku unapaswa kuwa na mpenzi wako. Chukua off kutoka kazini.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo unahitajika kufanya katika siku ya Valentine’s day.

#1 Anza na kiamsha kinywa ukiwa kitandani.

Kupata kiamsha kinywa kitandani ni jambo ambalo linaonekana kifahari. So anza siku yako kwa kuamka polepole ili usimuamshe mpenzi wako. Ingia jikoni umuandalie kiamsha kinywa ambacho anakipenda zaidi. Hakikisha ya kuwa ukishamaliza kupika unaosha vyombo vyote ili usimpe kazi yeyote atakapoamka.

Weka kiamsha kinywa kando yake halafu umuamshe polepole kwa kumbusu. Kama kuna ua ambalo ushalinunua tayari unaweza kumnukisha ili aamke na furaha.

#2 Ogeni pamoja.

Baada ya kunywa kiamsha kinywa, ni wakati wa nyinyi wawili kuenda kuoga. Maji moto ni njia nzuri ya kuwachangamsha ili siku yenu iwaendee vyema. Kama mumezoea kuoga pamoja, unaweza kuleta utofauti wa kuoga, unaweza kumwambia, “bebi leo nataka nikusugue mgongo”

#3 Angalieni filamu.

Baada ya nyinyi wawili kuvaa nguo, ni wakati wa kukaa kwa kochi huku mnagusana. Wekeni filamu ya kimahaba ambayo nyinyi wawili mnapenda. Kama inawezekana, mnaeza kuenda katika sinema kuangalia filamu ya mapenzi ambayo bila shaka atapenda. Kumbuka ya kuwa lengo lako siku ya leo ni kumtosheleza mpenzi wako, na wala si kujitosheleza. [Soma: 

#4 Chamcha mle sehemu ya wazi.

Kula katika sehemu iliyowazi ina starehe zake. So baada ya kuangalia filamu, mpeleke mpenzi wako kula chakula cha mchana katika sehemu iliyo wazi. Unaweza kuenda katika mkahawa unaoujua halafu uagize sehemu ambayo unayaona mazingira kwa upana. Kama haitawezekana, unaweza kuchukua hatua ya zaidi kufanya picnic. Mpeleke sehemu ya hifadhi yeyote, tandika mkeka, toa vinywaji na chakula cha mchana. Bila shaka atafurahi.

#5 Hifadhi kumbukumbu ya siku hio.

Baada ya kuspend muda mkiwa pamoja na kukula chakula cha mchana, mnapaswa kurudi nyumbani. Usijisumbue kutaka kufanya mengi siku hii ya Valentines Day. Pia usiharakishe mambo, fanya mambo polepole na kwa utulivu. Wakati mkiwa nyumbani mnabarizi, toa kamera yako na uanze kuchukua video ya vitu ambavyo nyinyi wawili mmefanya siku hii. Kumbukumbu hizi mtaziweka na mtakuja kuzikumbuka miaka ya usoni. [Soma: Jinsi ya kumuomba mwanamke atoke out na wewe]

#6 Washa mshumaa.

Watu wengi huhusisha siku hii na uwashaji wa mishumaa. Hivyo nawe usiachwe nyuma. Agiza chakula kutoka nje na upange mishumaa kadhaa kwa meza. Kama haitawezekana, unaweza kumpeleka katika hoteli yeyote ambayo imetenga siku hii kuwa spesho kwa Valentine’s Day ili kusherehekea. Msithubutu kuruka hatua hii ya kula chakula cha jioni bila kuwasha mishumaa, hata kama nyote wawili mmechoka. Hatua hii ni muhimu kwa kuwa inaifanya siku nzima kuwa kamili.

#7 Na mwisho kabisa…

Mkishamaliza chajio, rudini nyumbani na mjitayarishe tayari ya kupumzika na kutomasana kwa kitanda. Kwanza mnaingia kuoga, tia vinywaji kidogo ili kuondoa kiu. Nendeni chumbani na mzime taa. Washeni mishumaa kadhaa chumbani na muinjoy usiku mzima kwa mlalano. Hakikisha usiku huu unakuwa bora zaidi kuliko usiku wowote ule.

Kivyovyote vile, mpenzi wako ataifurahia siku hii kwa kuwa atajiona spesho. Siku hii ukiipanga kama tulivyokueleza basi mpenzi wako atakushukuru na atafall na wewe zaidi ya vile ambavyo hukua unatarajia.

Jiulize unataka mwanamkegani mwaishani mwako

Wadada wengi wanaolia kisa mahaba,,,wengi wao ni wale wanaopenda wakaka/wanaume wa show off yaani wanaolelewa na wazazi wao,,,
Wewe unashoboka na mwanaume/mkaka anayelala kwa mama yake hata akikujaza mimba hana pa kukupeleka wala hawezi kukuhudumia,,,,,
Na msipojielewa mtaishia kuwa mabango ya shabaha za mapenzi mpaka kiama,,,,
Tulia weka malengo unataka aina gani ya mwanaume maishani mwako na akija angalia ana mahitaji yako.

Share this:

Design a site like this with WordPress.com
Get started